Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri
WAKIHABIMA inawatakia wote sikukuu njema ya Christmas na mwaka mpya. Ni matumaini ya WAKIHABIMA kuwa mwaka ujao utakuwa ni wenye heri na mafanikio.

WAKIHABIMA imefanikisha ulipwaji wa mishahara ya vibarua 19 waliokuwa wamefanya kazi

na kushindwa kupata mishahara yao kwa wakati tangu May-Juni 2015. wafanyakazi hao walikuwa wamefanya kazi ya kusafisha uwanja wa ndege Masasi na kuahidiwa kulipwa bila mafanikio.

kwa mujibu wa wasaidizi wa kisheria, Donald Simonje na Mwinda Mkwamba waliosimamia mchakato wa ufuatiliaji wa haki hizo kisheria, wafanyakazi hao walikuwa mara zote wakiahidiwa

bila mafanikio wa ahadi zilizokuwa hazina mwisho. Naye kiongozi wa vibarua hao Bw. Yusufu Madonji walikuwa wana hali ngumu sana kimaisha kwani wengi walikuwa na madeni makubwa. Aidha alitoa shukrani kwa niaba ya wenzake na kuwaalika watu wengine wenye shida mbalimbali za kisheria kuja kwenye ofisi ya WAKIHABIMA ili kupata usaidizi. 

 

WAKIHABIMA kwa kushirikiana na shirika la legal services facility LSF litaendesha mafunzo ya siku moja ya namna ya kuandaa na kuandika andiko la mradi, project write -up. Mafunzo hayo yatafanyika siku ya tarehe 22/11/2016 kenye ukumbi wa kanisa Katoliki parokia ya Masasi mjini. Hii ni kwa mujibu wa maelezo ya mwenyekiti wa WAKIHABIMA, Mr. Fungafunga bada ya kupewa taarifa ya mafunzo hayo. Ni matarajio ya uongozi na wanachama wote kuwa mafunzo haya yatatoa mwanga wa kuwezesha asasi yetu kueza kuandaa maandiko ya miradi ili kupata wahisani watakaofadhili shughuli za asasi.

Hamjambo! WAKIHABIMA ilipata mwaliko wa kuhudhuria kongamano la wasaidizi wa kisheria lilioandaliwa na shirika la Legal Services Foundation (LSF) huko Dodoma kuanzia tarehe 24- 25 Oktoba 2016. WAKIHABIMA kwenye kongamano hili ilipeleka wawakilishi 2; Mr Tanmoza Fungafunga- M/kiti na Bibi Mwanaafa Wadi Malenga- Mjumbe wa k/tendaji. Ni Matarajio ya kila mwana WAKIHABIMA kuwa sasa shirika letu litakuwa limefunguliwa milango zaidi ya mafanikio.

Kikao cha kamati ya utendaji kimeamua kuanzisha darasa lingine lanutoaji wa haki za binadamu

kwenye kata ya Mwena yakilenga utoaji wa elimu ya haki za wanawake na watoto.

Msimamizi wa maunzo wa shirika Bi Tecla Mbawala amebainisha kuwa kazi ya usajili wa washiriki itaanza ambapo Bw. Maurice Ng'hitu amepewa kujumu la kuorodhesha majina. 

Kwa mara nyingine tena WAKIHABIMA ilipokea ugeni wa wafuatiliaji wa shughuli za kiasasi

toka LSF ambao walikutana na wanufaika wa huduma za WAKIHABIMA. Wageni hawa Shadrack Maluli na Esther kilembe waliweza kuongea na wananchi 10 (Me 6/ke 4) viongozi wa kata, afisa maendeleo ya jamii na wazee wa baraza la kata ya Mwenge Mtapika.

Wakati kwenye kata ya Mkomaindo wananchi 10 pia walitoa ushuhuda wa manufaa waliyopata toka asasi yetu na hapa pia viongozi wa mitaa (wenyeviti na watendaji)walitoa uzoefu wao wa kuifahamu asasi yetu na huduma zinazotolewa. 

Kwa ujumla ziara yao ilikuwa ya mafanikio ambayo tunaamini yatasaidia pia asasi yetu kupata mawazo na ushauri wa kutuwezesha kuendelea na huduma yetu kwa jamii.

Yale mafunzo ya ufahamu wa sheria kwa jamii yameanza 1/4/2016 kwenye kata ya Mwenge Mtapika ambako washiriki 25 toka mitaa ya Mbonde na Mayula wanashiriki. Mafunzo haya yamelenga kutoa ufahamu wa sheria za msingi: Sheria ya ardhi no 4&5 ya 1999, sheria ya mtoto na malezi, sheria ya ndoa ya 1971, sheria ya mirathi, sheria ya jinai na kazi na ajira. 

Kwa ujumla maendeleo na mahudhurio ni mazuri sana licha ya changamoto za hali ya hewa, mwingiliano wa shughuli za kijamii na sikukuu. Programu iliyopo ni ya kukutana kila alhamisi kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 na yatadumu kwa miezi 3 hadi mwezi Juni 2016.

Wawezeshaji ni WAKIHABIMA wenyewe kwa kutumia stadi walizofundishwa na ujuzi walionao katika masuala ya usaidizi wa kisheria na haki za binadamu.  

Wakihabima imeanza mwaka 2016 kwa kuanzisha mpango wa utoaji elimu ya ufahamu wa sheria kwa jamii. Mafunzo hayo yatafanyika kwenye kata ya Mwenge Mtapika ambapo jumla yawashiriki 20 watasajiliwa. Aidha mafunzo ya utetezi wa haki za wanawake yataanza mwezi April kwenye kata ya Nanganga. Huko washiriki 15 watapatiwa stadi za utetezi wa haki hiyo ni kwa mujibu wa msimamizi wake Paralegal Mwinda Mkwamba.