Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAFUNZO YA JKT KWA WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA NI KUWEKA MATABAKA.

Itakumbukwa kuwa ongezeko la idadi ya watu Tanzania ni kubwa sana,na miongoni mwao ni vijana, wakati serikali inakabiliwa na changamoto ya kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwahakikishia elimu ilio bora limekuja wazo la kuwapeleka vijana JKT kwa mujibu wa sheria, vijana hawa ni wale tu waliofaulu kidato cha sita wakapata daraja la kwanza na la pili na wale waliopata daraja la tatu kwa michipuo ya sayansi. Kundi hili ni dogo sana  ukilinganisha na idadi ya vijana waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka 2013 tu.

Mafunzo ya JKT ni muhimu kwa watanzania wote kutokana na faida zinazotokana na mafunzo haya, kwa ufupi tu mafunzo ya JKT humfanya kijana aweze kufanya kazi au kuishi katika mazingira yoyote ambayo binadamu anaishi, yanamfanya kijana kuwa na utii na kujali watu kikamilifu pia yanafanya kijana kuweza kujitegemea na kukabiliana na shida mabalimbali zinazomkabili na zaidi mafunzo haya huongeza uzalendo kwa raia. Hizi ni baadhi tu ya faida zinazopatikana kwa mtu binafsi. Lakini zipo faida ambazo taifa linaweza kuwa nazo kama vijana wake wanapatiwa mafunzo haya, mfano kuwa na taifa lenye watu waliokuwa tayari kwa ulinzi wa taifa lao, kuzalisha mali kwa gharama nafuu kwa kutumia askari vijana waliopo makambini na kuboreka kwa huduma zinazotolewa na waajiriwa ambao wamepitiamafunzo haya ambao hujali muda na wateja wao wanaowahudumia.

Faida hizi na nyingine nyingi serikali iliziona na ndio maana ikaweka mpango huu ambao hatujui kama utakuwa endelevu na kama utakuwa endelevu, je? Utakuwa endelevu kwa makundi yapi yaani yenye sifa zipi? Kwa utekelezaji unavyoendelea hivi sasa mpango huu mzuri na wa kizarendo kwa taifa letu utaleta matabaka makubwa mawili ambayo ni hatari kwa usalama wa taifa hapo baadae. Serikali inabidi ikumbuke kuwa mpango huu umeanza 2013 na ni kwa wanafunzi baadhi tu ya waliofaulu kidato cha sita, hivyo ni kundi dogo sana kwa kuwa tunajua wapowaliofeli na wapo walio faulu na waliofeli ambao ni wa miaka ya nyuma na hili ndilo kundi kubwa sana.

Tunaishukuru sana serikali kuurudisha mpango huu muhimu na mzuri kwa taifa letu hasa ukilinganisha na changamoto zinazolikabili taifa hivi sasa, changamoto za uuzaji, usafirishaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, ushabiki wa kisiasa, rasilimali, uwajibikaji mdogo na ongezeko la watu. Mpango huu unaweza kugusa kila aina ya changamoto hizi na kuzipunguza kwa kiwango kizuri sana lakini tu kama kutakuwa na uwiano wa kuwapeleka mafunzo haya ya kijeshi vijana wote wenye fursa na wasio na fursa, nikiwa na maana wale weye sifa za kujiunga na vyuo na wale wengine wowote waliopo majumbani na mitaani bila shughuli yoyote. Kwa kufanya hivi hatutaweza kulijenga taifa lenye matabaka ya walio na uwezo na wasio na uwezo. Tunajua upungufu wa rasilimali zinazoweza kuwezesha makundi haya yote kwenda jeshini, lakini serikali inaweza kuanza kwa awamu nusu wakachukuliwa wale tu waliopata fursa ya kumaliza kidato cha sita na nusu wengine wale ambao hawakupata fursa ya kufika kidato cha sita yaani darasa la saba na wote waliofeli kidato cha nne. Hivi tunaweza tukaenda mpaka tukafika wakati uwezo wa kuwapeleka makundi yote haya mawili walioko mitaani na wanaomaliza kidato cha sita ikawezekana.

Kwa kuendelea kuchukua wanaofaulu kidato cha sita peke yake na kuwaacha wengi waliofeli darasa la saba na kidato cha nne na waliofeli kidato cha sita jumuisha na waliokuwapo tiyari mitaani toka miaka ya nyuma, huku ni kuweka MATABAKA ambayo dhahili yatakuwa yanatofautiana KIUCHUMI na KIELIMU. Vijana  ambao wameishia darasa la saba na wamefeli kidato cha nne wakipatiwa mafunzo ya JKT ni fursa kubwa sana kwao, maana wanaweza kujiunga na makampuni ya ulinzi, wanaweza kujishughulisha na kilimo au ujasilia mali, wengine wanaweza kujiendeleza kielimu na fursa nyingine nyingi ambazo wanaweza kuzipata kutokna na cheti au mafunzo ya JKT, hali kadhalika kwa wanao maliza kidato cha sita na kukosa nafasi za kuendelea na elimu ya vyuo. Lakini kundi hili likiachwa ni kujitengenezea migogoro na migomo na hali ngumu ya maisha kwa vijana hawa, tunaona  na tutaendelea kuona ongezeko la vijana wanaotumia madawa ya kulevya, miashara ya ngono, wizi,ujambazi na hata ugaidi. Taifa litakuwa halina amani na halite tulia, serikali itatumia gharama kubwa katika kuimalisha ulinzi na kutawala watu wake lenyewe. Wakati kundi hili la wasomi na lililopata fursa ya kupitia JKT litakuwa na uwezo kiuchumi na elimu, na makundi haya mawili hayataweza kukaa katika mtaa mmoja kwa kuwa yatakuwa makundi hasimu nao pia watatumia gharama kubwa kuishi kwaajili ya kuijiimalishia ulinzi na usalama wa wao na familia zao. Inawezekana serikali ilianzisha mpango huu ikiwa inataka kumaliza kwa haraka tatizo la migomo ya vyuo vikuu iliyoibuka miaka ya hivi karibuni ama kuboresha utoaji wa huduma katika taasisi za serikali, lakini hilo sio suluhisho pekee, suluhisho la jumla ni kuhakikisha makundi yote ya vijana waliopata fursa ya kusoma na amabo hawa kupata fursa hiyo wana kwenda kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa uwiano ulio sawa na kwa hivyo ili nchi iwe na amani ya kweli ni razima kuwe na usawa katika mgawanyo wa rasilimali na fursa, kulingana na nafasi waliokuwa nayo raia sehemu husika.

Maoni yangu katika mpango huu wa serikali kupitia Jeshi la kujenga taifa ni kuhakikisha kwanza vijana wote wasio kuwa na kazi na hawakusoma na wapo wanazurula mitaani wanapelekwa jeshini kwa mujibu wa sheria  ili kupunguza matatizo mengi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yanayoweza kutokea katika jamii, ndipo wafuate wasomi ambao nao tunakubali ni lazima wakahudhuria mafunzo haya ilikuboresha utoaji wa  huduma za jamii. Serikali itakapo kuwa na rasilimali za kutosha makundi haya yawe yana kwenda katika mafunzo ya JKT kwa uwiano ulio sawa au mpango huu kwa sasa utekelezwe moja kwa moja kwa uwiano sawa kwa makundi haya makubwa mawili yote kwenda jeshini kwa pamoja, kuliko inavyo fanyika hivi sasa huku ni kuweka matabaka katika jamii ya watanzania ambao ni wamoja na wanatenganishwa katika huo umoja kwa mifumo kama hii isiyochambuliwa kwa kina kabla ya utekelezaji wake.

Wenu,

Deogratius Makoti

MWANAHARAKATI WA MASWALA YA VIJANA NA AFYA.

Mob: 0714113952/0782956772

27 Septemba, 2013
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

ABDULLAH MSANGI (GEITA) alisema:
sababu ya kuwapeleka hawa vijana JKT haiko wazi kihivyo sana kwani wanafundisha hawa vijana mbinu nyingi na aplication zero sasa basi tuanaomba hizo gharama za training zibadilishwe kwani wanapata ujuzi wasioutumia hizo fedha zikajenge maabara kwa sasa wakishajua wakifanya training watawapeleka wapi basi waendelee na zoezi lao sio kututafutia taabu wimbi la wezi ugaidi usio na kikomo,na makundi mengi ya kihalifu yasiyokuwa na mipaka
6 Desemba, 2014

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.