UWAMKI ni shirika la kiraia lililoanzishwa mwaka 2010 na wajasiliamali wazalendo wanaofanyakazi za mikono maeneo kijitonyama mpakani-B Dar es salaam. kwa wakati huo limekuwa likiongozwa na bw. Hansen magari ambae ni mwanziiishi mkuu.shirika lilianzishwa kwa lengo la kuleta mshikamano hata baadae liwe benk au ushirika wa maeneo hayo. na baadae mnamo mwaka april 2012 ndipo kamati teule ikasajiliwa wizara ya mambo ya ndani na kupewa cheti rasmi kma asasi ya kiraia na yenye ndoto na mipango tele ya maendeleo ya jamii katika eneo hilo na nchini kwa ujumla.