Parts of this page are in Swahili. View in English · Edit translations
UVIKITWE GROUP, kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society, imefanikiwa kutekeleza mradi wa uelimishajirika kwa vijana kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya na uhusiano wake na maambukizi ya VVU/UKIMWI. Mradi huu umetekalezwa katika wilaya ya Bagamoyo ndani ya kata sita ambazo ni Vigwaza,Chalinze,Ubena,Msata,Miono na Kiwangwa. Mradi huu umeweza kuwafikia vijana tisini (90) wanaotumia na wasiotumia dawa za kulevya.
Mafanikio ya mradi
- Kuanzishwa na kusajiliwa kwa CBOs kumi (10) zinazo toa elimu hii kwa jamii.
- Vijana wapatao 12 waliokuwa wanatumia dawa za kulevya , wameweza kujitambua na kuachamatumizi ya dawa za kulevya
- Vijana wanne 4 wameweza kuteuliwa na kuingia kwenye kamati za ukimwi za kata na kuwakilsha kwenye kamati za WODC ngazi ya kata
Changamoto tulizokutana nazo.
- Mahitaji ya jamii husika kuwa juu kuliko uwezo wa taasisi
- Uhitaji wa elimu ya stadi za maisha kwa jamii yote, kama nyenzo ya kuleta mabadiliko ya tabia.
- Wilaya ya Bagamoyo kuwa njia kuu ya kuingiza dawa za kulevya kutoka Zanzibara, ambako ndiyo njia kuu ya kuingizia dawa za kulevya kutoka nchi za nje.
B
Picha za baadhi ya vijana wa kata za mradi waliohudhuria mafunzo ya elimurika kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya na uhusiano wake na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
January 23, 2012
Comments (2)