Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

TUINUANE COMMUNITY ORGANIZATION.

MPANGOKAZI 2016/2021

1.UTANGULIZI                              

TUINUANE ni asasi iliyoanzishwa mnamo tarehe21 March 2012 na kusajiliwa kufanya kazi zake katika Manispaa ya Bukoba, namba yake ya usajili ni BMC/KCJ/12/869

Lengo na madhumuni ya asasi hii ni kuondoa au kupiga vita umaskini uliokithiri miongoni mwa jamii hasa kuanzia katika ngazi ya familia.

TUINUANE itawashirikisha wananchi katika kuwajengea uwezo wa ufahamu juu ya utambuzi, kuibua matatizo ndani ya jamii husika na kutafuta njia mbadala ya kukabiliana nayo.

Aidha asasi hii itaandaa mipango shirikishi kijamii yenye kuzingatia mahitaji na vipaumbele na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo, kufanya tathimini kabla ya na baada ya utekelezaji wa programu na hivyo kuwepo kwa miradi endelevu yenye kuleta mabadiliko yanayotarajiwa ndani ya jamii.

TAFSIRI

TUINUANE katika tafsiri yake ni ushirikiano wenye lengo la kuwafanya wahusika kuwa katika hali sawa ya kimaisha, hivyo wahusika wanaamua kwa pamoja kufanya jitihada za makusudi kukwamuana kutoka hali duni na kuwa bora zaidi.

TUINUANE inatambua haki na wajibu wa kushiriki na kushirikishwa katika kujenga ufahamu na namna ya kutatua tatizo linalomkabili kila mtu kwa nafasi yake.

DIRA

-      Kuwa na asasi yenye ubunifu wa hali ya juu na utatuzi wa mambo yote yanayokinzana na maendeleo na ustawi wa watu.

DHAMILA

-      Kuwashirikisha wadau wote wa maendeleo kuinua hali duni ya maisha kuanzia ngazi za familia na Taifa kwa ujumla.

 

MALENGO NA KAZI ZITAKAZOFANYIKA

TUINUANE inatarajia kutekelelza program zake katikaManispaa ya Bukoba.

Asasi yetu itatoa uamusho wa ufahamu kwa jamii vijana ,wanawake na wanaume juu ya kuanzisha na uimarishaji na uboreshaji wa kazi (ajira) walizonazo na pale inapowezekana wasaidiwe namna ya kubuni kazi mpya ambazo hazijaguswa na wananchi kwenye mazingira yao.

UFUGAJI, KILIMO, USINDIKAJI, SANAA, MICHEZO,UJASILIAMALI NA UFUNDI ni miongoni mwa shughuli zitakazopewa kipaumbele ili kuondokana na tatizo la ajira na umasikini.

Asasi itawawezesha vijana na wanawake kusimika moyo (Ari ya kutochagua kazi) ili mradi iwe kazi halali na itakayompatia kipato cha uhakika. Tutawajengea uwezo wa kujiamini, watawezeshwa na kuwaongezea elimu ya ujasiliamali kama njia bora ya kufikia ndoto za maendeleo.

 

I: SABABU INAYOPELEKEA PROGRAM/MIRADI ITEKELEZWE KWA SASA

Ukosefu wa ajira /kazi miongoni mwa vijana ni tatizo katika jamii yetu,kuwepo kwa kundi kubwa la vijana wanaozurura, wanaoshinda “vijiweni” kwa makundi makundi, wakicheza kamari, pool, karata/draft na wengine wakinywa pombe kali ya (viroba ) wakati wa saa za kufanyakazi.

Hii ndiyo sababu kubwa inayotulazimu TUINUANE kushawishika na kujitosa kusaidia juhudi zinazofanywa na serikali na kwa pamoja tuweze kutatua na kutafuta ufumbuzi suala la ukosefu wa kazi kwa wanawake na vijana.

Aidha takwimu za Manispaa ya Bukoba zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya vijana wanaomaliza darasa la 7 hawaendelei na elimu ya sekondari. Ni asilimia 0.1% ya vijana waliomaliza darasa la saba ndio wanaojiunga na vyuo kama VETA. Hivyo asilimia 99.9% wanaingia katika ajira isiyorasmi au hawapati ajira kabisa.

Vijana wengine vijijini hawana mwamko wa kazi za ufundi mchundo, za kuvuja jasho na kuthubutu kufanya kazi za ujasiliamali na hivyo hukimbilia mjini na kuongeza tatizo la uzurulaji.

Wengi hulazimisha kutafuta kazi za kuajiriwa serikalini au kwenye sekta binafsi, hata kama hawana elimu ya kutosha yenye sifa ya vyeti. Wanaposhindwa hawapo tayari kujifunza kazi za ufundi na za kuvuja jasho, ni vema sasa kuwashawishi kujiunga na ufundi na ujasiriamali kwa kuwatafutia nafasi za masomo k.m. VETA, SIDO au kwa mafundi uashi binafsi.

 

Kama tusikiavyo KAEMP,KADETFU,KCU,WORLD VISION,nk Ndivyo na TUINUANE yaelekea kuwa. Ila bado ni changa . Imeanza na vikoba sasa imetaka kuongeza kasi yake katika Nyanja nyingine ili tuweze kufaidi kasi hii yabidi jamii tukae na tuamue TUINUANE itusaidie nini baada ya kuchambua matatizo yetu katika mazingira magumu.  

 

TUINUANE inayo malengo mazito ambayo yamewekwa baada ya kuona hali yetu .Mipango ya 2016/21 ndani ya mtaa/Manispaa ni kulenga kubadilisha harakati za hali tuliyonayo ili tuwe na maisha bora katika kila fani, TUINUANE haiwezi kufanikisha lolote iwapo wanajamii hatuko tayari.Pia sisi ndio tupendekeze lipi tunahitaji au lipi litangulie kuliko mengineyo.Basi kuna umuhimu wa kutafiti kero zinazotusibu katika mtaa wetu/Manispaa ili tuelewe ni mchango gani tunaweza kuutoa au kuhitaji kutoka kwa wafadhili wa ndani au nje.

 

2.BAADHI YA MATATIZO NDANI YA MTAA/MANISPAA YA BUKOBA.

Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ambayo TUINUANE imegundua ndani ya MTAA/MAMISPAA .

*Ukosefu wa mitaji ya biashara na miradi midogo na mikubwa.  

*Uchumi duni katika ngazi ya kaya      

*Kukosa akiba ya fedha au chakula nyumbani.

*Migogoro ya kifamilia .                                        

*Vijana hawaendi Sekondari au Ufundi .                        

*Ajira imekosa Vijana wanalandalanda mtaan

 *Ukosefu wa Viwanda vya kusindika vyakula

*Ukosefu wa elimu ya ujasiliamali                            

*Ushiriki duni katika mipango ya maendeleo.                                

*Ongezeko la watoto wa mtaani na yatima.                                                   

 *Unyanyasaji kwa Wenye ulemavu na wakongwe

*Mashirika na wafadhiri hatuwafaidi kama mashirika mengine                                                    

*Maambukizi ya Ukimwi yanaongezeka.                                            

*Semina za Maendeleo na Miradi ni kidogo.                              

*Hatujatembelea walioendelea ndani/nje ya Bukoba/Tanzania.                                                                    

*Kutotakiana mafanikio bado ni kero.                                                                        *Ulevi,Ngonozembe,Magonvi bado ni changamoto

*Uwajibikaji duni wa viongozi katika kutafuta haki za raia wao.                                                                                                

 *Wawekezaji toka nje bado hawatoshi.

Upotevu wa mila na desturi

3.MIPANGO YA TUINUANE .

Baada ya TUINUANE kutumia wadau na kugundua kero zetu,tayari imedhamilia kushirikisha jamii kufanya mipango yao kuleta mabadiriko na kuelekea hali bora katika miaka mitano ijayo, 2016/21.Kazi hii siyo rahisi,yahitaji mipango madhubuti na kila mtu kuwajibika vilivyo.

TUINUANE inaamini kuwa kila mwenye akili,uhuru na utashi anaweza kubuni na kuleta maisha mapya.

 

4.LENGO:KUWEKA NA KUKOPA

Hatari na kiboko cha umaskini kwa watu wa hali ya chini ni SACCOS yaani Chama cha Kuweka na Kukopa.                     .                                                        

Ili kukwepa na kusahau kero nyingi, TUINUANE inaalika wanajamii kushiriki uanzishwaji wa SACCOS mapema , Utaratibu na uendeshaji wa SACCOC utaelezwa na wataalamu.Kinachohitajika ni utayari wa kila mtu kushiriki uanachama huku akiwa na lengo la kuinua kipato chake binafsi na familia yake kwa ujumla.                                                

 

FAIDA ZA KUSHIRIKI SACCOS:                                                          

*Kupata mtaji nafuu wa kilimo,biashara,ufugaji hadi kusomesha watoto au huduma za afya.                                        

*Uwezekano wa kupata semina na warsha za maendeleo binafsi na jamii au mazingira.                                                                                              

  *Kuongeza ushirikiano au marafiki zaidi tokana na ushirika huu wa kuinuana.                                                                 

  *SACCOS itakuwezesha kutembelea sehemu nyingi ndani na nje ya Wilaya.                                                                                                  

  *SACCOS itasaidia tupate huduma nyingineyo kama duka, Zahanati,mashine ya kusaga nafaka,viwanda vidogo vidogo.                                                                                                       

  *SACCOS itachangia maendeleo binafsi na jamii kiujumla.                                                

TUINUANE GROUP inataka ukweli na uwazi ili kila mtu ashirikishwe kikamilifu katika mpango kazi.                                                    

Mashirika mengi kama CREDIT kulitokea kuboresha mashamba yao,kutembea ndani/nje ya mazingira huku wanafarijiana licha ya kuongeza Elimu na uelewa wa mbinu mbalimbali za kujikimu kimaisha.

 

TUINUANE inapenda wazee wasaidiwe na kuthaminika hasa huku wanatoa maarifa yao kwa kizazi kipya kwa kurithisha tamaduni za kiasili.

 

(b)WATU WENYE ULEMAVU:Walemavu ni wa aina nyingi na hawa wote wanastahili haki sawa na watu wengine.                                                                                                                                              Pamoja na yote TUINUANE inakumbusha jamii iwahudumie wagonjwa na kushiriki katika shida na raha kama msingi wa Asasi hii.

                                                                                                         (C)YATIMANAWAJANE:                                                                                                            Hili ni kundi linaloongezeka hasa sababu ya UKIMWI.Ni wajibu wa kila mwana jamii kutambua kuwa Ukimwi ni tatizo na jamii ilizungumzie kila pembe na kudhibiti fursa zote zinazoendekeza tatizo hili .

 

TUINUANE ingependa tuwajali wajane na yatima wenye shida ndani ya jamii yetu,yatima wapate mahitaji kama watoto wenye wazazi tukitanguliza upendo na huduma kwao.

TUINUANE itasomesha yatima wakishirikiana na jamii inayowazunguka kwa misaada ya ndani na nje pale itakapowezekana . Akina mama na wajane wanavyovipaji vingi hasa uzalishaji,kazi za mikono kuchangiana nguvu/fedha,hii itapewa kipaumbele katika mafunzo mbalimbali yatakayotolewa na Asasi hii.

TUINUANE imeunda mtandao wa kutumia rasilimali wanawake wainuke kiuchumi/maendeleo huku wanafarijiana. Mwanamke ni nguzo ya familia yabidi wawezeshwe kwa njia ya semina,matembezi na ushindani ndani/nje ili waibukie kubadili sura ya kipato cha familia.

(d)VIJANA WA MTAA WA NYAKANYASI.                                                                                  Vijana ndio tegemeo la Jamii popote duniani maana ndio wana nguvu za kuleta mabadiriko ya haraka.Ni kundi lenye sauti katika Serikali,Siasa ,Dini, Maendeleo,Michezo/Burudani hata ndani ya familia.                                                                                                                    

 

TUINUANE inataka umoja wa vijana ili kuwezesha stadi,ajira,michezo kuthamini kilimo/ufugaji na biashara kwa njia ya kitaalamu.

 

8.LENGO V:DARASA LA UFUNDI;                                                                    

Vijana ambao hawakwenda Sekondari wanahitaji ajira au kuajiliwa.Wanapashwa kufundishwa stadi mblimbali kama ufundi seremala,uashi,ushonaji,kazi za mikono,mapishi bora na maarifa ya nyumbani.Pia upo umuhim kuelimisha juu ya kilimo bora ,ufugaji na mbinu nzuri za miradi/biashara.

Vijana wapanuke upeo baada ya kuzuru sehem za ndani/nje ya mazingira.

Watashiriki michezo,mashindano,midahalo,semina /warsha huku wanakutana na fikra tofauti kutoka kwa watu mbalimbali.  

 

9.MKAKATI WA KUSTAWISHA MALENGO YA TUINUANE KWA 2016/21                                                                                                                               TUINUANE, ingependa Kasi mpya,Ari mpya na Nguvu mpya viguse kila mlengwa wa maendeleo.Ni wakati wa watu wote kuamka kwa namna yake ili wawezeshwe kuonja utamu wa maendeleo ya kisasa.Itakuwa furaha ya TUINUANE kila mtu akiishi mazingira bora,lishe inayofaa,afya nzuri,ustaarabu kuepuka maambukizi ya Ukimwi,kushiriki utandawazi kuwa na akiba,amani ya roho,uhusiano mwema na jirani kuishi uraia na imani za kidini licha ya kupokea mabadiriko ili kuendana na wakati.                                                                              Ufanisi wa mipango ya TUINUANE utategemea mwamko wa jamii pindi wametambua kero na kuanza mkakati wa kuleta mabadiliko kiasi.

Mwamko wa maendeleo unategemea sana uelewa wa wananchi kuona tatizo wenyewe,kulitafutia ufumbuzi kwa njia shirikishi.Basi TUINUANE ipo nyuma ya wote wenye mapenzi mema.

Ili tufikie malengo tegemewa inabidi jamii iwe na wakereketwa kimaendeleo,watu wawe na uchu wa kubadirika kwa ubunifu na moyo wa ushindani.                                                          

 

 

MPANGO KAZI

SHUGHULI ZITAKAZOFANYIKA (MAFUNZO/ UWEZESHAJI)

S/N

SHUGHULI

LENGO

MASOMO/SOMO

WALENGWA

MUDA

GHARAMA

MATOKEO TARAJIWA

  1.  

Nadharia kuhusu ujasiriamali

Kuwajengea uwezo washiriki juu ya Nadharia ya ujasiliamali na jinsi ya mjasiriamali au kikundi jasiriamali kinavyoweza kutumia stadi za ujasiriamali kutambua fursa zilizopo na kuzitumia kuazisha biashara yenye mafanikio na itakayodumu.

  • Ujasiriamali ni nini.
  • Stadi za ujasiriamali.
  • Mahitaji muhimu ili mtu aweze kuwa mjasiriamali
  • Manufaa/faida za ujasiriamali.
  •  

Vijana (wasichana wavulana).

Wanawake na

Wanaume.

01June 2016- Dec2016

Toka kwa wahisani na Halmashauri/Manispaa

  • Kuongeza ajira na wajasiliamali
  • Kupatikana kwa uhisani na ruzuku
  1.  

Semina juu ya mazingira

KUTUNZA MAZINGRA KUWAFUNDSHA ATHALI YA KUHARIBU MAZINGRA UKATAJI MITI VYANZO VYA MAJI

  • UTUNZAJI MAZINGRA VYANZO MITI JAMII KUIUNGANISHA IWE NA UPENDO NA UMOJA WA KIMAEDELEO KURUDISHA AMANI

Vijana

Jan2017-Jun2017

 

Toka kwa wahisani na Halmashauri/Manispaa

Kuelewa tabia na mabadiliko ya nchi na kuendesha kilimo na mavuno bora

  1.  

Ubunifu (Kutambua fursa zilizopo na shughuli zinazoweza kuongeza kipato na faida).

Kubainisha ruzuku toka serikali kuu na wafadhili toka nje na jamuhuri ya muungano wa tanzania

Kuandaa maandiko ya miradi kulingana na fursa na ruzuku dhidi ya aina ya jamii husika

Vijana,wanawake na wanaume

July-2018-Dec 2018

Toka kwa wahisani na Halmashauri

Mfano,ACWW,

KOICA,TFR

Kupata miradi iliyowezeshwa mitaji na vyenzo na ushauri mtambuka.

  1.  

Mafunzo kwa vitendo, Shughuli za kilimo nabiashara za kijasiriamali

Lengo la somo: kuwawezesha wakulima waelewe kilimo cha biashara, pia tofauti ya mfanyabiashara wa kawaida na mjasiriamali, WALIO FANIKIWA

  • Kupata wazo la biashara MAENDELEO
  • Kutambua fursa zabiashara
  • Kutathimini na kubaini fursa mbalimbali zinazojitokeza katika kilimo na klimo cha biashara.

Vijana,wanawake na wanaume

Jan 2019-Jun 2019

Toka kwa wahisani na Halmashauri

Mfano,ACWW,

KOICA,TFR,

FAO,AGRA,TACri,

Rocfella foundation of America,TanzDevTrust

Kupatikana mazao bora na chakula cha kutosha na kipato stahiki.

 

  1.  

Elimu ya masoko

Lengo la somo: kuwezesha wanajamii/ wanakikundi/ wajasiriamali waelewe umuhimu wa elimu ya masoko katika kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za masomo. Uchumi wa soko huru, ushindani na jinsi ya kukabiliana nao. Ustadi wa kununua na kuuza uhusiano na wateja n.k.

  • Umuhimu wa taarifa za soko.
  • Utafiti wa soko.
  • Uchumi wa soko huru.
  • Ushindani na jinsi ya kukabiliana nao
  • Jinsi ya kuukabili ushindani
  • Ubora
  • Nguvu kazi
  • Utafiti wa soko
  • Mambo 5 ya kuzingatia katika kuzitafutia soko bidhaa zako

Vijana wanawake na wanaume katika eneo la mradi

July 2019-

Dec 2019

Toka kwa wafadhili na Halmashauri/Manispaa

 

Kupatikana kwa soko tijifu lenye kuleta kipato kwa wananchi na ushuru kwa serikali

  1.  

Nadharia kuhusu mpango wa biashara

Nadharia kuhusu mpango wa biashara

  • Maana ya biashara na
  • Kutayarisha mpango wa biashara.

Vijana wanawake na wanaume katika eneo la mradi

Jan2020-

Jun, 2020

Toka kwa wahisani na Halmashauri

 

Kupatikana kwa soko tijifu lenye kuleta kipato kwa wananchi na ushuru kwa serikali

  1.  

Mkakati wa kuandaa mpango wa biashara kwa shughuli za vikundi (Women and youth economic empowerment groups for IGA)

Lengo: vijana na wanawake wabuni kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali na kuboresha kipato.

  • Maana ya vikundi vya uzalishaji kiuchumi.
  • Namna ya kuanzishamfuko wa kuweka na kukopa (vikoba)

Vijana wanawake na wanaume katika eneo la mradi

July 2020

Dec 2020

 

Toka kwa wahisani na Halmashauri

 

 

 

 

vijana na wanawake kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali na kujiajiri na kuboresha kipato.

 

  1.  

Kufufua maadili mema katika jamii

Kufufua na kurejesha maadili mema kwenyejamii na kupunguza vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

  • Huduma za kiroho na ushauri nasaha kwa wenye maradhi (VVU)
  • Kutoa huduma za kiroho na wokovu na kurejesha imani thabiti ya kumcha Mungu

Watu wote ndani ya jamii.

Jan2021-Jun 2021

 

 

Kurejesha matumaini,jamii kukubali kubadili mienendo,tabia ya kumhofu MUNGU na kuwepo kwa imanithabiti na Amani

  1.  

Mazingira rafiki na elimu kwa ujumla wake

 

  • Namna ya kuanzisha na miradi ya utunzaji/uhifadhi mazingira.
  • Uhifadhi wa vyanzo asilia vya maji (traditional water sources)
  • Upandaji miti rafiki wa maji

 

July2021-Dec2012

 

Kuwepo miradi ya uifadhi mazingira k.m

Vitalu (miche),

Kuboreka visima asilia vya maji safi.

Kuboreka kwa

Afya na kupungua maradhi ya kuambukiza.

 

 

 

 

MATOKEO TARAJIWA YA TUINUANE GROUP NDANI YA JAMII WAKATI WA KUTEKELEZA PROGRAMU HII

 

MATOKEO YA KATI

VIASHIRIA

  1. Kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa jamii, kupitia mikutano ya ushawishi na uhamasishaji utakao tekelezwa na TUINUANE GROUP USHAWISHI, UHAMASISHAJI NA UTETEZI/KUIMARISHA AMANIN NA UPENDO KTK JAMII KUPUNGUZA/KUEPUSHA MIGOGORO KERO KUIFADHI MAZINGA MARA.KWANI PENYEUPENDO KUNA AMANI NA PENYE AMANI KUNA MAENDELEO
  • Idadi kubwa ya vijana na wanawake watakaojitokeza kushirikikikamilifu katika kuchangia nguvukazi za maendeleo.
  • Jamii kwa ujumla hasa vijana na wanawake watapata uamusho na kukubali kushiriki kazi za kuvuja jasho, kwa kutumia rasilimali watu na fedha zilizopo ndani ya jamii.
  • Jamii hasa vijana watapata uelewa wa kutosha na kuchanganua ajira na ajira zisizorasmi zinazolipa kwa manufaa yao.
  • Kutakuwa na kupungua fikra za uzururaji, kupungua kwa uvivu.
  • Vijana wengi wataiga na kujifunza toka kwa watu wakaothubutu kuanzisha miradi endelevu
  1. Kuongezeka kwa kipato na uwezo wa kumudu kulipia mahitaji muhimu ya msingi miongoni mwa vijana na wanawake.
  • Idadi ya vijana wakatakaothubutu kuanzisha na kutekeleza miradi midogomidogo ya kuongezakipato na hivyo vijana wengi kuonekana wanafanya kazi za kuvuja jasho.BDII
  • Kupungua kwa makundi ya uzururaji na ya vijiweni na vitendo vingine k.m. kucheza kamari kuvut a bangi nk.KUJIUNGA NA MAKUNDI ATALI
  • Vijana wataibua matatizo na mahitaji yao na kuweka vipaumbele katika kupata suluhisho la ukosefu wa kazi (Ajira) na kipato duni.
  1. Kuongeze kwa uelewa juu ya elimu ya ujasiliamali na miongoni mwa vijana na wanawake kwa kujiwekeamalengo ya muda mfupi na mrefu ya kuwa wajasirimali wanaojituma.
  • Vijana na wanawake watakao kuwa tayari kufanya kazi za ujasiliamali kwa mpangilio maalum, hawatakata tama katika kutatua matatizo yanayowakabili.
  • Watahamasishana wao kwa wao na watakuwa tayari kwa mabadiliko na watakuwa wepesi wa kugundua fursa za kibiashara zilizopo na kujiunga na makundi ya IGA
  • Jumuiya au vilabu vya biashara.
  1. Kuongezeka kwa watu wenye imani thabiti miongoni mwa vijana na wanawake.
  • Idadi ya watu wenye kuacha kabisa matendo yanayoenda kinyume na maadili UBAKAJI MAUAJI NK TUTAWAJENGA KUMUESHMU MUNGU ndani ya jamii na kumcha Mungu kikamilifu.