FCS Narrative Report
Utangulizi
Tanzania Albino Society
TAS - LINDI
Kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kuelewa Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu
FCS/RSG/3/09/188
Tarehe: Januari 01, 2011 - Machi 31, 2011. | Kipindi cha Robo mwaka: Kwanza |
Mhe. Salum Khalfan Barwany
S.L.P. 268
LINDI.
Tel: +255 23 220
Mob. +255 719 662 132
Barua Pepe: barwanys@yahoo.com
S.L.P. 268
LINDI.
Tel: +255 23 220
Mob. +255 719 662 132
Barua Pepe: barwanys@yahoo.com
Maelezo ya Mradi
Sera
Mradi ulilenga kujenga uwezo na uelewa kwa watu wenye ulemavu wakiwamo walemavu wa ngozi pamoja na jamii kiujumla kuhusu Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu ili watambue haki na wajibu wao katika michakato ya maendeleo. Mradi umetekelezwa katika Kata 5 za Manispaa ya Lindi ambazo ni; Mingoyo, Ng'apa, Makonde, Ndoro na Msinjahili zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi. Mradi umewezesha na kusaidia kuongezeka kwa uelewa wa watu wenye ulemavu wakiwamo walemavu wa ngozi (Albino) na jamii kiujumla kuhusu haki na wajibu wa watu wenye ulemavu katika michakato ya maendeleo kwa mujibu wa Sera husika. Mradi ulitekelezwa kwa kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa kuhusu Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu iliyofanyika mnamo tarehe 03 - 05/01/2011 na kushirikisha walemavu, watendaji wa kata, vijiji/mitaa na madiwani wapatao kati ya 42 hadi 45 kutoka katika maeneo ya utekelezaji wa mradi idadi ambayo ni ziada ya watu kati ya 6 hadi 9 ikilinganishwa na idadi iliyokusudiwa ambayo ni walengwa 36. Mradi pia ulifanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi katika maeneo husika kwa kuwashirikisha walengwa na wadau wa mradi wapatao 20 na kufanya tathmini shirikishi wadau ya mwisho wa utekelezaji wa mradi ili kubaini mafanikio, mapungufu, changamoto na mipango ya baadae ya kuendeleza matunda ya mradi husika.
Mkoa | Wilaya | Kata | Vijiji | Idadi ya Wanufaika |
---|---|---|---|---|
Lindi | Lindi Manispaa | Mingoyo, Makonde, Ndoro, Msinjahili na Ng'apa. | - | 330 |
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | |
---|---|---|
Wanawake | 33 | 98 |
Wanaume | 49 | 148 |
Jumla | 82 | 246 |
Shughuli na Matokeo ya Mradi
1. Kuongezeka kwa uwezo na uelewa wa Watu wenye ulemavu wapatao 36 wa kata 5 za Wilaya ya Lindi kuhusu Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu.
2. Kuimarika na kuboreka kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya Sera na maendeleo katika ngazi tofauti za jamii.
3. Kuongezeka kwa utambuzi, kudai, kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu kushiriki katika michakato ya kisera na kimaendeleo katika jamii.

1. Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa kwa watu wenye ulemavu 36 juu ya Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu kutoka kata 5 za Wilaya ya Lindi ifikapo Juni 2010.
2. Kufanya ufuatiliaji shirikishi wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi.
3. Kufanya tathmini shirikishi wadau ya mwisho wa utekelezaji wa mradi.
4. Gharama za utawala na uendeshaji wa mradi.
2. Kufanya ufuatiliaji shirikishi wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi.
3. Kufanya tathmini shirikishi wadau ya mwisho wa utekelezaji wa mradi.
4. Gharama za utawala na uendeshaji wa mradi.
1. Watu wenye ulemavu wakiwamo walemavu wa ngozi na wadau wa maendeleo wapatao 45 kutoka kata 5 za Lindi Manispaa wamejengewa na kuongezewa uwezo na uelewa kuhusu Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu.
2. Watendaji wa Serikali za Mitaa ngazi ya Kata, Vijiji/Mitaa na Madiwani wapata0 10 wa Kata 5 za Lindi Manispaa wamewezesha kufahamu wajibu, haki na nafasi ya watu wenye ulemavu katika michakato ya sera na maendeleo na kuimarika kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika vikao rasmi kama vile; Kamati za Maendeleo za Kata (KAMAKA/WDC)
3. Ushiriki wa watu wenye ulemavu na jamii wapatao 20 katika kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwenye kata 5 za mradi zilizopo katika Manispaa ya Lindi umeimarika na kuboreka.
4. Ushiriki wa watu wenye ulemavu na wadau wengine wapatao 20 wa kata 5 za Mradi zilizopo kwenye Manispaa ya Lindi katika kufanya tathmini shirikishi jamii ya mwisho wa utekelezaji wa mradi umezingatiwa, kuimarishwa na kuboreshwa.

Tofauti iliyojitokeza ni kuongezeka kwa idadi ya washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu kutoka watu 36 iliyokusudiwa na kufikia 45 kama ilivyokuwa katika uhalisia wake.
1. Kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa kwa watu wenye ulemavu 36 juu ya Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu kutoka kata 5 za Wilaya ya Lindi (TZS. 3,323,000/=)
2. Kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi (TZS. 576,000/=)
3. Kufanya tathmini shirikishi wadau ya mwisho wa utkelezaji wa mradi (TZS. 805,000/=)
4. Gharama za utawala na uendeshaji wa mradi (TZS. 259,000/=)

Mafanikio au Matunda ya Mradi
1. Kuongezeka kwa uelewa wa watu wenye ulemavu na jamii kiujumla kuhusu haki, wajibu, nafasi na fursa zilizopo na kuwazunguka za kujiletea maendeleo kwa mujibu wa sera.
2. Kuongezeka na kuboreka kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya sera na maendeleo kwenye ngazi tofauti za msingi katika jamii.
3. Kuboreka kwa ushirikiano kati ya taasisi za Serikali, Asasi Zisizo za Serikali, viongozi wa dini na asasi nyinginezo dhidi ya asasi za watu wenye ulemavu.
4. Kupungua kwa vitendo vya unyanyapaa tofauti dhidi ya watu wenye ulemavu kutoka kwa jamii inayowazunguka.
5. Kuongezeka kwa idadi ya uandikishaji shule watoto wenye ulemavu walio chini ya umri wa miaka mitano (5) katika maeneo tofauti ya halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

Kuongezeka kwa uelewa wa watu wenye ulemavu na jamii kiujumla kuhusu haki, wajibu, nafasi na fursa zilizopo na kuwazunguka za kujiletea maendeleo kwa mujibu wa sera.
2. Kuongezeka na kuboreka kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya sera na maendeleo kwenye ngazi tofauti za msingi katika jamii.
3. Kuboreka kwa ushirikiano kati ya taasisi za Serikali, Asasi Zisizo za Serikali, viongozi wa dini na asasi nyinginezo dhidi ya asasi za watu wenye ulemavu.
4. Kupungua kwa vitendo vya unyanyapaa tofauti dhidi ya watu wenye ulemavu kutoka kwa jamii inayowazunguka.
5. Kuongezeka kwa idadi ya uandikishaji shule watoto wenye ulemavu walio chini ya umri wa miaka mitano (5) katika maeneo tofauti ya halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
2. Kuongezeka na kuboreka kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya sera na maendeleo kwenye ngazi tofauti za msingi katika jamii.
3. Kuboreka kwa ushirikiano kati ya taasisi za Serikali, Asasi Zisizo za Serikali, viongozi wa dini na asasi nyinginezo dhidi ya asasi za watu wenye ulemavu.
4. Kupungua kwa vitendo vya unyanyapaa tofauti dhidi ya watu wenye ulemavu kutoka kwa jamii inayowazunguka.
5. Kuongezeka kwa idadi ya uandikishaji shule watoto wenye ulemavu walio chini ya umri wa miaka mitano (5) katika maeneo tofauti ya halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
1. Kuimarika kwa mahusiano na ushirikiano miongoni mwa watu wenye ulemavu wenyewe.
2. Kupungua kwa vitendo vya kunyanyapaa na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu katika masuala na michakato ya kisera na kimaendeleo katika maeneo yao.
2. Kupungua kwa vitendo vya kunyanyapaa na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu katika masuala na michakato ya kisera na kimaendeleo katika maeneo yao.
Hakuna sababu zozote za mabadiliko.
Mambo Mliyojifunza
Maelezo |
---|
Watu wenye ulemavu wamesahaulika katika kujengewa uwezo na uelewa kuhusu Sera na Sheria mbalimbali zinazolenga kulinda na kutetea haki zao. |
Watu wenye ulemavu hawajapatiwa nafasi na fursa ya kutosha ya kushiriki kikamilifu katika machakato mbalimbali ya kimaendeleo. |
Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo hawajakidhi haja na mahitaji ya watu wenye ulemavu kujiwezesha kujiletea maendeleo wao wenyewe. |
Watu wengi wenye ulemavu hawana kabisa na/au wana kiwango duni cha elimu hali inayosababisha na kupelekea kushindwa kukabiliana na mazingira yanayowazuguka na changamoto mbalimbali za kimaendeleo. |
Jamii bado ina mtizamo hasi na potofu kuhusu haki, wajibu na nafasi ya watu wenye ulemavu kiushiriki kikamilifu katika michakato tauti ya maendelo. |
Kukosekana kwa muda mrefu na kucheleweshwa utungaji na utekelezaji wa Sheria Na. 10 ya 2010 ya Watu Wenye Ulemavu imepelekea utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Watu wenye ulemavu kufanyika kutokana na matakwa na utashi wa mtu mmoja mmoja badala ya kuwa kwa mujibu ya sheria halali za nchi. |
Changamoto
Changamoto | Namna mlivyokabiliana nazo |
---|---|
Watu wenye ulemavu wengi kuwa na kiwango duni au kukosa kabisa elimu iliyo rasmi. | Mafunzo yaliendeshwa kwa kutumia zaidi mbinu shirikishi za uwezeshaji. |
Kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu katika jamii ikilinganishwa na uwezo wa mradi kuwafikia walengwa. | Watu wenye ulemavu walioshiriki mafunzo kuhamasishwa kuwajengea uwezo na uelewa wenzao kuhusu Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu. |
Kukosekana kwa sheria ya watu wenye ulemavu hali inayopelekea Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu kutotekelezwa kabisa au kutekelezwa kwa mapungufu makubwa. | Kuwahamasisha watu wenye ulemavu na wanaharakati wengine kuunganisha nguvu na sauti ili kuhimiza Serikali na wadau wengine utekelezaji wa Sheria Na. 10 ya 2010 ya Walemavu |
Jamii kukosa mwamko na hamasa ya kuwasaidia na kuwawezesha watu wenye ulemavu katika nyanja tofauti za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. | Kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua, kulinda na kutetea haki na wajibu wa watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo. |
Watu wenye ulemavu kukosa uwezo na uelewa wa kutosha kuhusu Sera ya Taifa ya Walemavu na Sheria mbalimbali zinazolenga kulinda na kutetea haki zao. | Watu wenye ulemavu walioshiriki mafunzo kuhamasishwa kuwajengea uwezo na uelewa wenzao kuhusu Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu. |
Kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu zikiwamo haki wa watu wenye ulemavu. | Kuelimisha na kuhamasisha jamii kulinda na kutetea haki za binadamu zikiwamo za watu wenye ulemavu. |
Watendaji wa Serikali za Mitaa ngazi ya Kata,Vijiji/Mitaa na Madiwani kutoelewa kabisa Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu hali inayopelekea haki wa watu wenye ulemavu kutosimamiwa kikamilifu. | Kuhamasisha watendaji wa Serikali za Mitaa pamoja na madiwani kusimamia kikamilifu haki za watu wenye ulemavu katika nyanja tofauti za kimaendeleo. |
Mahusiano
Wadau | Namna mlivyoshirikiana nayo |
---|---|
Madiwani, Watendaji wa Kata, Vijiji/Mitaa | Kuhudhuria mafunzo ya Sera ya Taifa ya Walemavu, kufungua mafunzo na kuelimisha jamii na kusimamia haki za watu wenye ulemavu katika nyanja tofauti. |
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKi) na Waandishi wa Habari | Kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu haki za binadamu na masuala ya maendeleo kiujumla na kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhusu haki wa watu wenye ulemavu. |
Viongozi wa Dini | Kuhudhuria mafunzo kuhusu Sera ya Taifa ya Walemavu na kuwaelimisha na kuwahamasisha waumini katika dini zao kutambua, kulinda na kutete haki za binadamu zikiwamo za watu wenye ulemavu sawa na Sera na Maandiko matakatifu. |
Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata na Wilaya | Kuhudhguria mafunzo na kuelimisha jamii kutambua, kulinda na kutetea haki za binadamu zikiwamo za watu wenye ulemavu. |
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa - Lindi | Kutoa kitabu cha Sera ya Taifa ya Walemavu na kuhudhuria mafunzo ya Sera ya Taifa ya Walemavu yaliyofanyika. |
Mipango ya Baadae
Shughuli Zilizopangwa | Mwezi wa 1 | Mwezi wa 2 | Mwezi wa 3 |
---|---|---|---|
Hakuna shughuli zilizopangwa kutekelezwa katika robo ijayo kwa kuwa mradi ni wa miezi mitatu (robo moja ya mwaka) | - | - | - |
Walengwa Waliofikiwa
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | ||
---|---|---|---|
Wajane na Wagane | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Wazee | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watoto Yatima | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watoto | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wenye Ulemavu | Wanawake | 19 | 65 |
Wanaume | 32 | 87 | |
Jumla | 51 | 152 | |
Vijana | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wengine | Wanawake | 14 | 33 |
Wanaume | 17 | 61 | |
Jumla | 31 | 94 |
(Hakuna jibu)
Matukio Mliyoyahudhuria
Aina ya Tukio | Lini | Mambo uliyojifunza | Hatua zilizochukuliwa |
---|---|---|---|
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku (MYG) | Februari, 2010 | Namna ya kutekeleza na kusimamia mradi kikamilifu na ipasavyo | Kutekeleza mradi kwa kuzingatia maarifa na stadi zilizowezeshwa |
Ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji Mradi | Aprili, 2011. | Namna ya kutekeleza na kusimamia mradi kikamilifu na ipasavyo na utunzaji wa kumbukumbu | Kufanya marekebisho ya utunzaji wa kumbukumbu za mradi na asasi kiujumla. |