Log in
TANZANIA ASSOCIATION FOR MENTALLY HANDICAPPED

TANZANIA ASSOCIATION FOR MENTALLY HANDICAPPED

Bukoba, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

UTANGULIZI

Mradi wa kujenga uwezo wa viongozi na wanachama wa TAMH-Kagera,ulipatikana kwa ufadhili wa THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY LTD yenye makao makuu Dar-es-salaam,Tanzania.Baada ya kurudi kutoka mafunzoni hukomwalisaini mkataba wa ruzuku ya kwanza ya Tshs.7,500,000 utekelezaji wa mradi ulianza rasmi tarehe 6/8/2012 - 18/8/2012

Mafanikio

(a) Hatua zote za mradi zilifuatwa na vikao vyote vya mafunzo vilifanyika

(b) Mahudhurio ya mafunzo yalikuwa mazuri kila siku .

(c) Wawezeshaji walijituma muda wote wa mafunzo washiriki waliuliza maswali na yote yalipata  majibu sahihi toka kwa wawezeshaji na wakati mwingine toka kwa washiriki wenyewe.

(d) Vitabu vya fedha vliandaliwa vyema na taratibu zote za uhasibu na usimamizi wa fedha zinafuatwa kwa mara ya kwanza baada ya mafunzo.

(e) Asasi ina mpango mkakati wa miaka miwili unaotekelezeka.

(f) Kwa sasa asasi ina computer na printer.

(g) Tathimini ilishirikisha watu wa nje wawili ambao walifurahishwa sana na kushangazwa namna mradi huu wa kwanza ulivyoendeshwa kwa mafanikio na ufanisi mkubwa.

Changamoto:

Watu wenye ulemavu wa akili kushindwa kujisemea au kujieleza wanapopata matatizo kwa asilimia 80% wanahitaji msaada wakati wote na hivyo kupunguza uwezekano wa kuwa wasemaji wa matatizo yao na haki zao.