Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Hivi sasa mradi wa lugha ya alama kwa wazazi wa viziwi na viziwi uliokuwa unaendeshwa katika wilaya 8 za mkoa wa Tanga umemalizika na mkataba kati ya CHAVITA NA FOUNDATION Umeshafungwa. kwa sasa CHAVITA Kipo katika mchakatowa kuandika mradi mwingine wa MKUKUTA.

Kwa upande mwengine CHAVITA kipo katika maanalizi ya mkutano mkuu wa mwaka 2011 utakaofanyika mapema mwezi ujao,hivyo mkutano huo utahusisha wanachama wote wa mkoa wa Tanga pamoja na matawi ya chavita yaliyopo katika wilaya za korogwe, muheza, lushoto,pangani,handeni,mkinga,kilindi, hivyo tunaomba wadau mbalimbali kutuunga mkono katika kutimiza azma yetu hiii ya kuleta demokrasia katika CHAVITA.

 

Na kwa mara ya kwanza chavita Tanga kwa kushirikiana na shirika la STARKEY HEARING FOUNDATION la nchini marekani limeandaa kutoa msaada wa vifaa vya kusaidia kuongeza usikivu kwa watu wote wenye matatizo ya kusikia katika wilaya zote 8 za mkoa wa Tanga, hivyo tunaomba wadau na serikali watusaidie kuhamashisha watu hao wajitokeze kwa kujiandikisha kwa maafisa maendeleo ya jamii na ofisa za CHAVITA katika wilaya husika na pia katika ofisi za wakuu wa wilaya na CHAVITA MKOANI ili kuweza kuwa na taarifa sahihi za watu wenye matatizo ya kusikia. vifaa hivyo vinatolewa bure.