Kabla ya kuja kwa wamishionari na waarabu hapa afrika,waafrika waliamini kuwa kuna Mungu ingawa imani yao hakuandikwa kwenye vitabu kama ilivyo kwa Biblia inayotumiwa na wakristo au Quran tukufu inayotumiwa na waislamu.Misingi ya umoja,ushirikiano na upendo ni kati ya mafunshisho ya dini za kiafrika.Kwa sasa katika karne hii ambayo mafundisho ya dini hizi za kigeni ndio yameshika kasi,maadili yanazidi kubomoka.Je ni vema kama tutatazama nyuma na kuurejea uafrika wetu na dini zetu?