Envaya

SHANGWE COUNSELING CENTRE

FCS Narrative Report

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

FCS Narrative Report

Utangulizi

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha Utawala bora kwa wanawake Vijijini.
FCS/MG/2/10/099
Tarehe: 1Sept, 2011- 31Nov, 2011Kipindi cha Robo mwaka: 3
Samuel Philimon Ngwipa ( Meneja Mradi).
P.o. Box 3101
Mbeya

Maelezo ya Mradi

Utawala Bora na Uwajibikaji
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu unalenga utoaji elimu wa haki za wanawake ambao ndio walengwa hasa wa mradi ikiwemo kuwashirikisha katika mipango mbalimbali ya maendeleo
MkoaWilayaKataVijijiIdadi ya Wanufaika
MbeyaRungweMpuguso,Kyimo,Bujela,Bulyaga,Kisondela na LufingoSimike,Kalalo,Itete,Iponjola, Lugombo, Kagwina, Bulyaga kati,Bugoba,Mtindo,Lutete, Kisuba,Ndubi,Mpombo,Katabe, Mibula,Bujela,Isaji,Ipumbuli,Isongola.60
 Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wanawake4511
Wanaume159
Jumla6020

Shughuli na Matokeo ya Mradi

Kufanyika kwa mkutano wa utetezi na uhamasishaji kwa wanawake 45 na wanaume 15 katika kata za Lufingo,Kyimo,Bujela,Kisondela,Mpuguso na Bulyaga
1.Mkutano wa uhamasishaji na utetezi juu ya haki za wanawake kwa wanawake na wanaume katika kata sita za Rungwe.
Mkutano wa utetezi na uhamasishaji juu ya haki za wanawake umeweza kufanyika tarehe 3Sept,2011.Jumla ya walengwa 60 wanawake 45 na wanaume 15 walishiriki katika mkutano huo. Masuala ya mila na desturi zinazowakandamiza wanawake yaliweza kushughulikiwa kwa kina mfano mgawanyo wa mali kwa mama Suzana wa Bulyaga ambaye kwa muda mrefu alikuwa akifuatilia sehemu yake ya urithi na hakuweza kupata uvumbuzi, katika mkutano huu alitoa hoja yake , kwakuwa Mkuu wa mila na desturi alihudhulia mkutano huu aliahidi kulishughulikia suala hili na kulipatia majibu
Hakuna Tofauti Yoyote.
Mkutano wa uhamasishaji juu ya haki za wanawake- 3,548,500/

Mafanikio au Matunda ya Mradi

Kiwango cha jamii kutambua haki za wanawake na kuheshimu mawazo ya mwanamke kuongezeka mfano katika kata ya Lufingo wanawake walipendekeza kuanzisha mradi wa ng,ombe wa maziwa kwa kusaidiwa na ofisi ya mifugo wilaya na mradi wa uanzishwaji wa mashamba ya chai, mawazo yao yalikubaliwa na viongozi wa vijiji na wilaya , na yanashughulikiwa ili kuanzisha miradi hiyo.
Vikundi vya maendeleo ya wanawake vimeweza kuanzishwa mfano kata ya Kisondela wanawake wameanzisha vikundi vya maendeleo (vicoba) kwa ajili ya kukabiliana na hali ngumu ya uchumi na kusaidiana wakati wa matatizo.
Wanawake wengi wamejitokeza katka kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na maendeleo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
Hakuna

Mambo Mliyojifunza

Maelezo
Shughuli za utetezi na uhamasishaji ni shughuli muhimu sana katika kutatua matatizo ya wanawake vijijini kwani bila kufanyiwa utetezi sauti zao hazisikilizwi na viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na watunga sera mfano katika shughuli za utetezi tuliyoifanya kulikuwepo na watu maarufu ambao ni rahisi kusikilizwa katika jamii, hivyo watu hao waliweza kuona umuhimu wa mwanamke na kuhamasisha jamii kuheshimu utu wa mwanamke, hivyo wanawake kupata nafuu mbalimbali za kimaisha.

Changamoto

ChangamotoNamna mlivyokabiliana nazo
Kuhamahama kwa viongozi wa serikali za vijiji wanaoujua mradi na ambao walishiriki kikamilifu katika mafunzo ya haki za wanawake na kuja wapya ambao inabidi tuanzenao mwanzo kuwaelekeza yale tunayoyafanya na pale tulipofikia Kuwapatia muhtsari na ripoti mbalimbali inayohusu mradi unaoendelea ili waufahamu vema na kuendelea kutoa ushirikiano

Mahusiano

WadauNamna mlivyoshirikiana nayo
Vituo vya sheria za haki za wanawake na watotoKutoa rufaa ya walengwa wanaohitaji msaada wa kisheria
Idara ya ustawi wa jamiiKutoa rufaa kwa ajili ya wanawake wanaohitaji misaada ya kijamii katika ngazi ya familia.

Mipango ya Baadae

Shughuli ZilizopangwaMwezi wa 1Mwezi wa 2Mwezi wa 3
Kufanya tathmini na warsha itakayojumuisha wadau mbalimbali katika kutathmini mradi uliofanyikaXXX

Walengwa Waliofikiwa

    Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wajane na WaganeWanawake(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Wanaume(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Jumla(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWIWanawake3(Hakuna jibu)
Wanaume1(Hakuna jibu)
Jumla4(Hakuna jibu)
WazeeWanawake(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Wanaume(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Jumla(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Watoto YatimaWanawake(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Wanaume(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Jumla(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
WatotoWanawake(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Wanaume(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Jumla(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Watu wenye UlemavuWanawake2(Hakuna jibu)
Wanaume2(Hakuna jibu)
Jumla4(Hakuna jibu)
VijanaWanawake(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Wanaume(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Jumla(Hakuna jibu)(Hakuna jibu)
Watu wengineWanawake4011
Wanaume129
Jumla5220
Hawa ni wawakilishi wa wanawake na wanaume waliohudhulia mkutano wa utetezi na uhamasishaji

Matukio Mliyoyahudhuria

Aina ya TukioLiniMambo uliyojifunzaHatua zilizochukuliwa
Usimamizi wa ruzukuOctober ,2011Namna ya kubadilishana uzoefu wa masuala ya Usimamizi wa fedha.Mkutano wa pamoja na kamati tendaji pamoja na watendaji ili kutoa mrejesho wa maagizo na mafunzo yaliyotolewa.

Viambatanisho

« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.