FCS Narrative Report
Utangulizi
SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha utawala bora kwa wanawake Vijijini.
FCS/MG/2/10/099
Tarehe: 23March,2011-23May,2011 | Kipindi cha Robo mwaka: 1 |
Samuel Philimon Ngwipa
P.o.Box 3101
Mbeya
Tel: 0764047354
P.o.Box 3101
Mbeya
Tel: 0764047354
Maelezo ya Mradi
Utawala Bora na Uwajibikaji
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu inalenga vipengele muhimu vya utawala bora kama vile utoaji elimu juu ya haki za wanawake katika jamii na uwajibikaji wa viongozi wa ngazi mbalimbali za vijiji na wilaya kwa ujumla katika kuwashirikisha wanawake kwenye masuala ya maendeleo yao.
Mkoa | Wilaya | Kata | Vijiji | Idadi ya Wanufaika |
---|---|---|---|---|
Mbeya | Rungwe | Mpuguso, Kisondela,Bulyaga,Bujela,Lufingo,Kyimo | Simike, Kalalo, Kagwina,Itete,Lugombo,Ipongola,Igalabwe, Bulyaga juu, Igamba, Bulyaga kati,Mtindo,Bugoba,Lutete,Kisuba,Ndubi,Kibatata,Nampuga,Ilenge,Isyukula,Kibisi,Kyimo, Katabe,Mibula,Ipumbuli,Isaji,Bujela,Isongola,Ipombo,Kyamandege,Segela | 150 |
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | |
---|---|---|
Wanawake | 93 | 682 |
Wanaume | 57 | 368 |
Jumla | 150 | 1050 |
Shughuli na Matokeo ya Mradi
Wanawake 93 na wanaume 57 wameweza kupata elimu juu ya utawala bora na haki za wanawake katika nyanja mbalimbali, na baada ya mafunzo hayo wanawake na wanaume hao wameanza kutoa elimu waliyoipata kwa jamii katika maeneo yao vijijini kwa kuzingatia mpango kazi walioupanga baada ya semina.
1. Kuendesha mafunzo juu ya haki za wanawake na utawala bora
2. Waliopata mafunzo yaani wakufunzi kutoa mafunzo katika vikundi mbalimbali vya kijamii
2. Waliopata mafunzo yaani wakufunzi kutoa mafunzo katika vikundi mbalimbali vya kijamii
kilichofanyika ni utoaji wa mafunzo juu ya utawala bora na haki za wanawake, ambayao yalitolewa kwa awamu tatu tofauti tarehe 4 April - 8April 2011, 11 April - 15 April 2011, 19 April - 23 April 2011 katika kata sita za wilaya ya Rungwe ambazo ni Mpuguso, Lufingo, Kyimo, Bujela, Bulyaga na Kisondela. Washiriki waliopata mafunzo haya ni wanawake .93 na wanaume 57 amabao waliandaa mpango kazi kwa ajili ya kutekeleza mradi..Baada ya Mafunzo wakufunzi mia moja walipewa vitini ili kuweza kuendesha mafunzo juu ya haki za wanawake katika vijiji vyao.Mafunzo hayo yalianza tarehe 10/5/2011 Masuala yaliyoshughulikiwa ni Wanawake 3 walionyang,anywa Mali baada ya waume zao kufariki Dunia, Msaada wa rufaa ya kwenda kituo cha sheria kwa Mwanamke mmoja toka Lufingo anayepigwa mara kwa mara na mumewe, Wanawake 2 katika kata ya Mpuguso waliobakwa na kushindwa kutoa taarifa popote kwa kuogopa kutengwa na wanajamii.Maelezo ya wanawake hao ya awali yamechukuliwa na kuwasilishwa kwenye kituo cha msaada wa kisheria Mbeya Mjini.
Hakuna Tofauti
mafunzo zilitumika 16,200,000/=
Wakufunzi kuendesha mafunzo katika vijiji vyao 3,600,000/=
Uandaaji wa vitini 750,000/=
Uandaaji wa washiriki 200,000/=
Manunuzi ya Pikipiki 1,850,000/=
Wakufunzi kuendesha mafunzo katika vijiji vyao 3,600,000/=
Uandaaji wa vitini 750,000/=
Uandaaji wa washiriki 200,000/=
Manunuzi ya Pikipiki 1,850,000/=
Mafanikio au Matunda ya Mradi
Wanawake walio katika mazingira duni na migogoro mbalimbali wamepata fursa ya kushiriki katika kutoa maamuzi kwa kuzingatia haki zao mfano wanawake 7 katika kata ya Bujela, Kisondela na Lufingo wamejiunga kwenye mabalaza ya ardhi ili kuhakikisha maslahi yao katika ardhi yanaangaliwa ipasavyo.
Wanaume wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kutambua na kuheshimu wanawake na haki zao kwani wao wenyewe wamekuwa hodari katika kuendesha mafunzo vijijini juu ya kuheshimu wanawake na haki zao, wameonyesha dhamira njema katika kutetea haki za wanawake ,badiliko hili si la kawaida kwa wanaume wa kabila la kinyakyusa ambalo kiwango cha mfumo dume ni kikubwa.
Badiliko jingine kubwa ni upande wa wanawake kuonyesha kujitambua wao wenyewe mfano mmoja ni kwa upande wa wanawake 3 wa kata ya Kyimo walioonyesha dhamira kubwa ya kuchukua hatua katika kudai ushiriki wao kwenye mabalaza ya kata na mabalaza ya ardhi, na kupewa nafasi hiyo.
HAKUNA
Mambo Mliyojifunza
Maelezo |
---|
Wazo jipya tulilolipata katika kutekeleza mradi huu ni kwamba wanaume wakipata elimu ya kweli na ya kutosha juu ya haki za wanawake wanabadilika na wanapata mwitikio mkubwa pindi wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwani hata wanaume wenzao huwasikiliza kuliko mwanamke kusikilizwa kutokana na hali ya dharau iliyojengeka katika jamii kwamba mwanamke hapaswi kusikilizwa, kwa hiyo wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwa mwanamke ni faida kubwa. |
Wazo jingine ni kwamba pamoja na harakati nyingi za ukombozi kwa mwanamke zinazoendeshwa na asasi mbalimbali Tanzania, bado hali ya mateso kwa mwanamke wa kijijini ni kubwa, wanawake bado wanabakwa, wanapigwa, wananyimwa nafasi za ushiriki katika mipango ya maendeleo, kiujumla hawasikilizwi, hivyo bado tunakazi kubwa ya kufikia Wilaya yote ya Rungwe hasa tukilenga kuelimisha wanaume na viongozi wa vijiji. |
Bado viongozi wengi wa vijiji ni madikteta, wananchi wananyanyaswa na kupewa adhabu na faini zisizo na msingi, mfano washiriki wawili waliochelewa mafunzo tuliyokuwa tukiendesha kwa sababu za kufiwa , Mtendaji aliposikia hawajafika kwenye mafunzo kesho yake walipokuja aliweza kuwapigisha magoti kwa muda mrefu na kuwaamuru warudishe posho walizopewa kwenye mafunzo na faini ya elfu kumi kila mmoja kwa ajili ya mgambo aliyewafuata, kwakweli kama shangwe tulikataa wale akinamama kuturudishia posho, lakini ile faini ya mgambo aliwaamuru watoe, kwa kweli wenzetu vijijini wanateseka na hawa viongozi wa kata na vijiji. Yaani viongozi hao wanaabudiwa ni mungu watu. |
Katika kutekeleza miradi mingine inayokuja , kama tutaendelea kuwa pamoja, tumegundua ni vema kutenga fungu la msaada wa kisheria kwa wanawake, kwani tumekutana na kesi nyingi za uonevu na manyanyaso juu ya wanawake zinazohitaji fedha kwa ajili ya msaada wa kisheria lakini tumekwama, japo kesi zingine zilizokuwa ni mbaya sana ilibidi tuchangie kutoka mifukoni mwetu ili kuweza kunusuru hali zilizokuwa zikiendelea. |
Jambo jingine muhimu tulilojifunza ni kuhamasisha wanasheria sasa kufungua matawi yao vijijini hasa wanasheria wanawake kwani mateso ya wanawake vijijini ni makubwa sana kuliko mjini ambako wanawake wengi mjini wanatambua haki zao, katika miradi ijayo tumeona vema kutenga fungu kwa ajili ya kuhamasisha wanasheria na watetezi wa haki waliopo mjini wakitafuta ajira wafungue matawi vijijini kazi zipo nyingi. |
Wanawake wa vijijini ni waelewa sana na wanakiu ya kujifunza na kutafiti mambo muhimu yanayoendelea katika Nchi yetu. |
Changamoto
Changamoto | Namna mlivyokabiliana nazo |
---|---|
Changamoto ya kwanza ni kwa ajili ya wanawake 30 waliokuwa wakihitaji msaada wa kisheria, ilikuja kugundulika kwamba ni kweli msaada wa kisheria ni bure kwa wanawake katika vituo kadhaa, lakini kuna mambo mengi yanayohitaji fedha, mfano nauli ya nenda rudi, malazi, chakula nk., mahitaji hayo hayakuwekwa kwenye bajeti | Tuliweza kuwasaidia wanawake wawili ambao kesi zao zilikuwa mbaya za kubakwa tulichangisha kiasi cha shilingi laki 340,000/=, kwani mmoja wao aliyebakwa alizaa mtoto ambaye pia alikuwa anahitaji huduma za matibabu, mpaka sasa kesi zao zinasimamiwa vema na mwansheria husika, japo mbakaji mmoja amekimbia mji. |
Kuchelewa kwa ruzuku kutoka FCS ambapo wanajamii waliona kwamba tunawadanganya na hivyo kutaka kuharibu kusudio zima la mradi. | Ruzuku ilifika na tulitekeleza mradi kama inavyotakiwa na hivyo tulimaliza changamoto hiyo na jamii ikafurahi. |
Wanawake vijijini kuwa na hofu pindi wanapofanyiwa ukatili hawawezi kusema , wakisema hutengwa hata na wanawake wenzao | Mafunzo yaliyoendeshwa yameweza kuwabadilisha na sasa wanaweza hata kujieleza mbele ya jamii. |
Mahusiano
Wadau | Namna mlivyoshirikiana nayo |
---|---|
Vyombo vya habari mfano ITV, NIPASHE NA MWANANCHI | Vyombo vya habali viliweza kurusha shughuli zetu hewani na kuufanya mradi kutambulika na jamii kubwa |
Serikali ya Tanzania | Mkuu wa Wilaya ya Rungwe ndiye aliyefungua mafunzo tuliyokuwa tukiendesha. Watendaji wa kata na vijiji waliweza kutoa ushirikiano mzuri katika kuwatambua washiriki waliopata mafunzo |
Vituo vya sheria | Tumeweza kushirikiana na kituo cha sheria Mbeya hasa katika kutoa rufaa ya kesi zinazohitaji msaada wa kisheria. |
Asasi zisizo za kiserikali mfano Planet Vision, Walter reed | Tumeweza kushirikiana nao katika kuchangia mawazo ya kuboresha shughuli mbalimbali za mradi unaoendelea. |
Mipango ya Baadae
Shughuli Zilizopangwa | Mwezi wa 1 | Mwezi wa 2 | Mwezi wa 3 |
---|---|---|---|
Kuendesha mkutano na viongozi wa vijiji na kata (60) ili kuhamasisha utetezi juu ya mwanamke hasa katika kuwasikiliza pindi wanapoleta malalamiko yanayohusisha uonevu na ukatili. | X | ||
Kufanya mchakato mzima wa ufuatiliaji | X | X | X |
Walengwa Waliofikiwa
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | ||
---|---|---|---|
Wajane na Wagane | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Wazee | Wanawake | (Hakuna jibu) | 23 |
Wanaume | (Hakuna jibu) | 11 | |
Jumla | 0 | 34 | |
Watoto Yatima | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watoto | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wenye Ulemavu | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Vijana | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wengine | Wanawake | 93 | 682 |
Wanaume | 57 | 368 | |
Jumla | 150 | 1050 |
NIL
Matukio Mliyoyahudhuria
Aina ya Tukio | Lini | Mambo uliyojifunza | Hatua zilizochukuliwa |
---|---|---|---|
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku | December 2010 | Maana ya bajeti na umuhimu wake, uchambuzi wa bajeti, uandishi wa taarifa,Usimamizi wa fedha,Mpango kazi wa mradi, uandaaji wa taarifa za fedha, uandaaji na uhifadhi wa vitabu vya fedha | Kuboresha taarifa za fedha na taarifa za shughuri za mradi. |
Tamasha la asasi za kiraia | 2007 | Kuheshimiwa kwa matakwa na sauti za wananchi ili kuepusha kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki | Kuelimisha wafanyakazi wa asasi na jamii juu ya umuhimu wa jumiya ya afrika mashariki |