Envaya

Scholars Focus Against Social Miseries

SFASM STUDENTS' STAND UP CAMPAIGN.

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

SFASM STUDENTS' STAND UP CAMPAIGN.

 

STUDENTS' STAND UP CAMPAIGN.

Students` Stand up campaign ni mpango wa kutoa elimu na kuhamasisha vijana hususan wanafunzi juu ya kukataa na kukemea vitendo vya rushwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi,Mpango huu ulianza rasmi katika shule ya Mayanga Sekondari mnamo tarehe 27/05/2011 chini ya SFASM kwa matarajio ya kuzifikia shule mbalimbali hasa maeneo ya Mtwara vijijini.Malengo makuu ya kuanzisha mpango huu ni kutaka kuwandaa na kuhamasisha vijana hasa Wanafunzi dhidi ya Rushwa na Maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kuwafanya kuwa mabalozi bora katika jamii walizotoka kuanzia ngazi ya familia mpaka ya kitaifa.Vilevile mpango huu umeambatana na malengo mengine ikiwemo kuhamasisha wanafunzi juu ya elimu kwa mfano kuzingatia masomo,namna ya kujifunza na kuongeza kiwango cha kufaulu kama tatizo kubwa kwa shule za nyanda za kusini.

3.0 TATHMINI.

3.1.wanafunzi.

Wanafunzi wa Mayanga walioudhuria semina hiyo iliyotolewa na waelimishaji kutoka SFASM juu ya “Student’s Stand Up Campaign” iliyolenga kuhamasisha ukemeaji wa vitendo vya Rushwa katika mazingira ya shuleni na jamii kwa ujumla.Wafunzi wa Mayanga walionesha msisimuko mkubwa wa hamasa kwamba elimu ya rushwa kupitia semina hii waliomba iwe endelevu kwa kushirikisha taasisi mbalimbali mfano SFASM pindi mada ya rushwa inapofundishwa shuleni

                                           

Picha(a), ni Wanafunzi wa Mayanga sekondari akichangia mawazo juu ya uelewa kuhusu mada ya rushwa na picha (b) Wanafunzi waliojibu vizuri wakipokea zawadi na SFASM

      Picha(C), ni Mwenyekiti wa SFASM Bw. Anthony Living (mwenye miwani) akiwatambulisha rasmi mabalozi (Wahabi Makacha kidato cha pili na Asma Kaluma kidato cha nne) watakaowakilisha SFASM kama kikundi cha wakemea rushwa shuleni hapo, Kutokana na kuhamasika na elimu juu ya rushwa Wanafunzi waliweza kubainisha mifano mbalimbali ya rushwa inayotendeka katika mazingira yao ya shuleni na kuahidi kukabiliana nayo

 3.2.Waalimu.

Waalimu wa wanafunzi hao pia walionesha ushirikiano wa karibu na waelimishaji (SFASM) katika kufanikisha mpango kazi ulioandaliwa kwa wanafunzi hao juu ya rushwa.Mbali na waalimu hao kukubali kuwa walezi wa kikundi hicho cha wapinga rushwa hapo shuleni, pia walipendekeza SFASM kuendelea na jitihada hizo za uhamasishaji katika shule mbalimbali hususan zilizopo maeneo ya vijijini.Hata hivyo Waalimu wa shule hiyo walipewa fursa ya kutoa hamasa na wito kwa wanafunzi wao juu ya rushwa na jinsi ya kuiepuka.

 3.4 SFASM.                                       

Tathmini ya kikundi cha Wanazuoni hawa          imegawanyika katika makundi mawili ikiwemo,(a) Tathmini juu ya utayari wa Wanafunzi na Waalimu katika mada ya rushwa (b) tathmini juu ya shule na mazingira ya ufundishaji.

Katika tathmini ya utayari juu ya mada,ilionekana bayana kuwa asilimia kubwa ya Wanafunzi walionekana kuhamasika na kuelewa vizuri mada kwa uthibitisho wa kujibu maswali mbalimbali kwa usahihi yalioulizwa na Waelimishaji.Maswali hayo yaliambatana na zawadi mbalimbali ikiwemo Madaftari,Peni,Rula na Majarida yenye ujumbe juu ya rushwa.

 

Picha (d), Wanafunzi wa shule ya Mayanga sekondari (Darasani) wakifuatilia mada ya rushwa kwa makini..

 

Tathmini katika Shule ya Mayanga inaonesha bayana kuwa mazingira ya ufundishaji hayatoi morali au hamasa kwa wanafunzi hao kuelewa masomo mbalimbali kwa kiwango kinachotarajiwa,kwa mfano somo la Uraia (Civics) ambalo kuna mada juu ya rushwa kwa kidato cha pili (kwa mujibu wa mtaala wa shule za sekondari Tanzania).Hivyo ukosekanaji wa vifaa vya ufundishaji ikiwemo Vitabu,Majarida vipeperushi na ufundishwaji wa vitendo inapelekea uwelewa mdogo kuhusu rushwa.

 4, Changamoto.

Mbali na jitihada mbalimbali zinazofanywa na SFASM katika uhamasishaji juu ya kukemea vitendo vya rushwa ikiwemo kwa kutumia vyombo vya habari(mfano kumuhamasisha kijana kukataa rushwa katika uchaguzi;mwaka 2010),kuandaa semina(mfano mashuleni), kushiriki katika mada mbalimbali (mfano siku ya Wanawake duniani, Machi 8/2011) mada kuu ikiwemo “Rushwa kikwazo kikubwa katika elimu kwa maendeleo ya

mwanamke”,changamoto mbalimbali zinazojitokeza zimekuwa zikirudisha malengo ya SFASM.Miongoni mwa changamoto ambazo SFASM imekuwa ikikabiliana nazo ni ukosefu wa fedha za kufanikisha malengo tuliojiwekea,dhana na vitendea kazi kama vile Kompyuta (Computer) ,Mafaili Chombo cha usafiri,Printa(Printer) na mashine ya kutolea nakala (Photocopy machine),

Ushirikiano na mwitikio mdogo kati ya Asasi za kiserikali na za kibinafsi kwa mfano,juu ya kuviwezesha vikundi mbalimbali hususan vinavyohusu kukemea vitendo vya rushwa na vilevile mtazamo usio sahihi wa wakazi kuhusu rushwa,ikichukuliwa kama tatizo lisiloweza kuachanishwa au kupunguzwa katika jamii.

 

Picha(d), Wahamasishaji wa SFASM wakasubiri chombo cha usafiri (Pikipiki) kituo cha Iyali (Mtwara vijijini) kuelekea shule ya Mayanga umbali wa kilometa tano toka hapo kituoni

5. Mafanikio.

SFASM Imeweza kupata mihaliko mbalimbali ili kushiriki kutoa mada ikiwemo ndani na nje ya chuo cha Mt.Augustino tawi la Mtwara,pia kwa kutumia vyombo vya habari na mijadala imeweza kutoa hamasa kubwa kwa vijana kuwa na mwitikio wa uhanaharakati ili kuimarisha nguvu kazi ya Taifa.Hata hivyo imeweza kupata uwelewa mkubwa kutoka katika dawati la uelimishaji ofisi ya TAKUKURU,

 6. Hitimisho..

Mbali na changamoto mbalimbali ambazo kikundi hiki(SFASM) kinazipata,kimejiwekea malengo ya kuikomboa jamii hususani kielimu kutokana na matatizo mbalimbali kama ilivyoelezwa hapo awali kwa tathmini ya kila miaka mitano tangu ilipoanzishwa rasmi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

September 26, 2011
Next »

Comments (3)

MWAKISOLE,Lusekelo (MTWARA) said:
I LIKE THAT,BIG UP AND I CONCUR WITH U GUYS,KEEP IT UP FOR SUSTAINABLE DEVELOPMENT.
October 27, 2011
LIVING said:
THANX MR MWAKISOLE
November 17, 2011
Chichidodo Paul (Dodoma) said:
Dah ebana bigup sana wadau. Mnaonyesha ukomavu kuwa nyie ni vijana wa leo. Katikati ya Jana na kesho hapo ndipo kuna muda, mnajua nazungumzia siku gani. bigup Sana Tonrash
November 21, 2011

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.