Envaya

PANGANI COAST CULTURAL TOURISM PROGRAMME

RAIS AVUTIWA NA BANDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

RAIS AVUTIWA NA BANDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. (Dkt)Jakaya Kikwete amelitembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya Kimataifa ya  biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam  na kujionea shuguli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo.  Mheshimiwa Rais aliyefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alionyeshwa kuvutiwa sana na kazi nzuri inayofanywa na Wizara sambasamba na kujionea bidhaa mbalimbali na kupata maelezo ya kina na ya kitaalamu kutoka kwa waoneshaji wa idara, taasisi na mashirika yaliyo chini ya wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania. Katika Banda hilo Rais Jakaya Kikwete alipata pia  fursa ya kucheza bao na mkewe mchezo wa asili wa bao ambao ni maarufu na unaochezwa na makabila mengi hapa nchini.

Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika pembe za ndovu ambazo ni miongoni mwa bidhaa zinazoonyeshwa katika banda la wizara ya Maliasili na Utalii. Kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Banda la wizra ya Maliasili na Utalii ambaye pia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Ibrahim Mussa.

Rais Kikwete akifuahia sanamu ya fisi ambayo ni moja vionyeshwa alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii


« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.