Je vijana wanahitaji nini ili waweze kujikwamua kimaisha?
Kwa hakika ni jambo jema sana kwa mtoto kukua na kuelekea kwenye hatua muhimu na kubwa kimaisha ya kuamua yeye anataka kuwa nani? kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Moja ya hatua ngumu na Nyepesi ni hatua ya Ujana ambayo ndio imekuwa dalaja la mafanikio kwa jamii nyingi ulimwenguni na pia Umasikini. Naomba nieleze dhana hizi mbili ya ugumu na urahisi wakati wa umri huu wa ujana , Tukianza na hali ya Ugumu kwa vijana, kuna changomoto nyingi sana zinazowakabili vijana kama hizi zifuatazo , MAPENZI NA NGONO, MADAWA YA KULEVYA, MARADHI KAMA UKIMWI, MKWAMO WA UCHUMI, KUKOSEKANA KWA AJIRA, NA N.K.... hapo ndipo utaona wa dhana ya ugumu kwa hatua ya ujana ambayo kijana anahitji kufanya kila linawezekana kukabiliana na hizo changamoto ili kuufanya ulimwengu uendelee. Sasa nini vijana wanahitaji ili kujikwamua na changammoto hizo nilizokwisha kuzitaja hapo mwanzo? Bila shaka ni NYENZO. Moja kwa moja nieleze Nyenzo ambazo vijana wanahitaji kukabiliana na changammoto hizo, Moja ya nyenzo muhimu sana ni ELIMU ... hakuna hata mmoja anaweza kushindana na changamoto tulizo nazo bila kuwa na siraha hii muhimu ya elimu kwa kila nyanja kwa mfano huwezi kujihusisha na ngono zembe kama una ufahamu wa kuwa kuna maradhi yanayotokana na ngonon zembe, nini kinachokusaidia kufahamu madhara ya ngono zembe ni elimu.