Envaya

large.jpg

wanavijiji wa kata ya Kabuku ndani wakiwa wanapitia na kujadili changamoto za kata yao haswa changamoto za mimba kwa wanafunzi wa shule za sekondari Wilayani Handeni

large.jpg

wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chogo wakijadili tatizo la mimba za utotoni/shuleni Wilayani Handeni.

 LENGO KUU LA MUYODE

Kutoa mchango katika juhudi za Serikali katika kuikwamua jamii katika matatizo ya kielimu, mazingira, uchumi, haki na kuwaepusha na magonjwa mbalimbali ya ngono hasa UKIMWI.

 MADHUMUNI YA MOYODE.

  • Kuunganisha nguvu na juhudi za jamii katika kujiletea maendeleo endelevu.
  • Kuiwezesha jamii kutambua thamani yake katika kutoa mchango wao katika kutatua matatizo mbalimbali.
  • Kuunganisha jamii na wataalamu mbalimbali ili kupata mbinu bora za kupambana na     umaskini na maradhi.
  • Kuanzisha program zitakazoifunza jamii kuwa raia wema na wenye maadili mema.
  • Kuinua vipaji vya watoto na vijana katika fani za sanaa, michezo na burudani kwa kuwa na eneo maalumu kwa ajili ya shughuli hizo.
  • Kushirikiana na wataalam, asasi za kiraia na za serikali ndani na nje ya nchi ili kusaidia   jamii ya kitanzania.
  • Kuendesha program zenye kuinua hali za kiuchumi, mazingira bora na zenye kubadili tabia       hatarishi kwa vijana na watoto kama matumizi ya dawa za kulevya, ngono zisizo salama na ubakaji. 

large.jpg

Mwenyekiti wa mwanambogo akiwa katika mkutano na walimu wa shule za msingi katika mkutano wa kujadili masuala ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za msingi