Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

 Fitina Haule-Mwanachama       Wilson Karuwesa-Mwachama

                                                     

 

Farida Msengwa-Mwanachama      Agnes Haule-Mwanachama

 

 

 

           

John Kidasi Mwanachama                  

 

 

 

                                                                             

                                                    Thadei Hafigwa-Mratibu                             

Hilda Singano-Mwanachama      Monica Liampawe-Mwanachama

                                                   

                                    

Latifa Ganzel Mwanachama                   

 

Devota Minja-Mwanachama

orodha ya wanachama wa Morogoro Press Club 

 

                                     

 

 

 

 

Mnamo Februari 29,2012 wawakilishi wa  MOROPC  walikutana na ujumbe wa balozi wa Sweden katika hotel ya Hilux ambapo wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni

Aziz Msuya

Abedi Dogoli

Thadei Hafigwa

Samuel Msuya

Kenneth Simbaya-Rais wa UTPC

Tumsifu Mmari-Mwakilishi ubalozi wa Sweden

Anders Emanuel- Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden

Kikao kilianza kwa Rais wa UTPC Kenneth Simbaya kutoa utambulisho kisha Bw.Anders Emanuel kutoka ubalozi wa Sweden alitaka kujua ni jinsi gani Klabu ya waandishi wa habari imeweza kuleta mabadiliko katika jamii ya watu wa Morogoro.

Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari walitaja kuwa maeneo mengi ambayo wameyafanyiwa kazi kwa manufaa ya wananchi,maeneo hayo ni Hospitali ya Mkoa, Elimu katika Mkoa wa Morogoro na Migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Katika hayo MOROPC walianza ziara ya kutembelea maeneo yasiyofika kiurahisi na kuwa sauti za watu ambazo hasikiki ikiwemo kutembelea shule ya sekondari Mikese. Shule ya sekondari Fulwe na Shule za msingi zilizo pembezoni mwa manispaa ya Morogoro kuweza kujionea changamoto zinazowakabili.

Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari walisema kuwa yapo mengi ambayo wameyafanya kwa manufaa ya wananchi ila waligusia maeneo matatu ambayo ni;

Hospitali ya Mkoa, Elimu katika Mkoa wa Morogoro na Migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

Katika mazungumzo hayo walianza kwa kuelezea ziara ya kutembelea maeneo yasiyofika kiurahisi hivyo MOROPC imekuwa msemaji wa makundi ya watu wasiokuwa na sauti(watu wanaoishi pembezoni mwa mji) ambao sauti zao hazisikiki.

Waandishi waliweza kutembelea shule ya sekondari Mikese,Shule ya Sekondari Fulwe na Shule za msingi zilizo pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro ikiwemo shule ya Sekondari ya Uluguru kuweza kujionea changamoto zinazowakabili.

Maeneo yafuatayo yameanishwa na MOROPC kwa ujumbe wa Ubalozi wa SIDA katika mazungumzo ya awali yaliongozwa na Rais wa UTPC Kenneth Simbaya;

AFYA

Katika eneo la afya MOROPC ilichukua jukumu la kufanya ziara katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro ambapo ilibainika kuwepo kwa matatizo mbalimbali wanayowakabili wagonjwa ikiwemo ucheleweshwaji wa kupatiwa huduma kutokana na madaktari kutokuwepo katika eneo la kazi,Wodi ya wazazi kuwa na wagonjwa wengi na wengine kulala chini na uchakavu wa chumba cha kuhifadhia maiti, uchakavu wa vyandarua na mashuka, ukosefu wa baiskeli za kubebea wagonjwa.

Aidha waandishi waliweza kuibua hali mbaya ya mazingira katika hospitali hiyo, ubovu wa jenereta la dharura wakati kunapokuwa hakuna umeme wa gridi ya Taifa , ukosefu wa chumba cha kufulia nguo.

Baada ya kubaini hayo MOROPC iliweka agenda ya kuandika habari za hospitali hiyo ya rufaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwa kipindi cha wiki moja mfululizo ikalazimu mkuu wa mkoa wa Morogoro kufanya ziara ya kustukiza na kubaini uzembe wa uwajibikaji katika Hospitali hiyo.

Kisha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood alifuatia kwa kufanya ziara katika hospitali hiyo ambapo naye alijionea matatizo hayo na kutoa msaada wa mashuka,sabuni na baiskeli za kubebea wagonjwa.

Hali hiyo iliufanya uongozi wa Mkoa kupitia kwa katibu tawala kuanza kuboresha miundo mbinu na kujengwa kwa chumba maalum cha kufulia nguo.

Hivyo, MOROPC inaamini kuwa kazi ya vyombo vya habari ilisaidia kutatua kero za wananchi ambao walikuwa hawana mtu wa kuwasemea jambo hilo ilipelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutoa shukrani kwa MOROPC kwa jitihada zake huku wengine wakitembelea ya MOROPC kutoa shukrani kutokana na habari hizo.

Mazingira hayo yamepelekea MOROPC kuamini kwa kutembea kifua mbele kwamba hayo ni matunda ya kazi yake baada ya kusikiliza kero za wananchi zilizokuwepo kwa muda mrefu bila ya kutatuliwa na kuzifanyika kazi.Hivyo baada ya waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa kuhabarisha umma serikali ilichukua hatua kwa kipindi kifupi na baadhi ya watendaji kuwajibishwa na baadhi kuhamishwa vituo vyao vya kazi.

ELIMU

Pia katika suala la elimu MOROPC iliandaa ziara katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari Uluguru, Shule ya msingi Fulwe na Shule ya sekondari Fulwe ambapo vigezo vilivyozingatiwa katika ziara hiyo ni kuangalia ujenzi wa majengo yanayojengwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi katika miradi ya MEM na MES na kubaini ya kuwa majengo mengi yamejengwa chini ya kiwango ambacho hakilingani na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

Mafanikio yalipatikana baada ya kuandikwa na kutangazwa kwa habari hizo kwa kamati ya ujenzi ya wilaya ilianza kufuatilia ujenzi ule na kuwabana wakandarasi waliojenga majengo chini ya kiwango kuyaboresha upya na mkandarasi kukagua mara kwa mara hatua moja baada ya nyingine wakati wa ujenzi.

MOROPC pia katika eneo hili imetimiza wajibu wake vema ambapo inajivunia kuwa imeweza kusaidia jamii kuwa na majengo bora yatakayodumu kwa muda mrefu,imesaidia kuwepo kwa uwajibikaji kwa viongozi wa serikali(accountability).

ARDHI

Katika suala la migogoro ya ardhi kulingana sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999 MOROPC imeweza kuwasaidia wananchi kwa kuripoti habari mbalimbali kuhusiana na migogoro kati ya wafugaji na wakulima hasa katika wilaya ya Kilosa ambapo tatizo kubwa lililoonekana ni kuwa Serikali haikuwa sahihi kutoa maamuzi yake katika migogoro hiyo ikiwemo kuwahamisha wafugaji bila ya kuwatengea eneo lao walipotakiwa waondoke katika wilaya ya Kilosa kwamba ni wapi walitakiwa kwenda.

MOROPC kwa kushirikiana na wadau wake wakubwa ambao ni UTPC na MCT iliendesha mkutano wa mahusiano mema kati ya waandishi wa habari,wakulima na wafugaji wa kutoka wilaya ya Kilosa baada ya kutokea hali ya sintofahamu miongoni mwao.

 

Utekelezaji wa shughuli hizo yameleta heshima kubwa kwa MOROPC kwa kutekeleza wajibu wake ambapo wadau mbalimbali wamekuwa na imani kubwa kwa MOROPC na washirika wake ambao ni UTPC na MCT.