Log in
Majani Natural and Scientific Health Promotions (MANSHEP)

Majani Natural and Scientific Health Promotions (MANSHEP)

Mbeya, Tanzania

Lishe bora na mlo kamili ni muhimu kwa afya kwani huongeza kinga ya mwili ya kukabiliana na magonjwa na kulainisha ngozi. Katika sehemu ambazo watu wanatumia matunda na mboga za majani kwa wingi matumizi ya dawa zenye kemikali zinazotengenezwa viwandani, yanapungua sana.

large.jpg

Vipodozi salama vya asili vinaweza kumfanya mtu kuwa mrembo na kuvutia bila kujihatarisha kiafya. Ni busara kuepuka vipodozi vyenye kemikali na sumu zinazoweza kusababisha kansa, kuharibika kwa figo/ini, ugumba, kuota ndevu kwa wanawake pamoja na matatizo ya afya ya akili (msongo)

large.jpg

Kansa ni tatizo linaloongezeka sana katika jamii ya Watanzania kutokana na kubadilika kwa mfumo wa maisha ya asili. Maisha ya kisasa hasa ulaji wa vyakula vilivyosindikwa kwa kemikali, huchangia ongezeko la tatizo hili, chukua tahadhari.

large.jpg

large.jpg

MATUFAA KWA AFYA,LISHE NA TIBA

An apple a day will keep the doctor away…An apple before bed makes the doctor beg his bread” (kula tunda moja la tufaa kila siku humfanya mtu asiwe na haja ya kuonana na daktari…kula tunda la tufaa kila siku humkosesha daktari mapato yake). Misemo hii ya Waingereza inaonyesha umuhimu wa matunda ya matufaa kwa ajili ya kudumisha afya ya binadamu, kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali. Matufaa yana Vitamini K, nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals) aina ya quercetin flavonoid.

Faida za kiafya

  • Matufaa ni tiba nzuri ya ugonjwa wa kuharisha.
  • Husaidia katika matibabu ya uvimbejoto wa utumbo (colitis)
  • Husaidia katika matibabu na kuzuia shinikizo la damu
  • Husaidia katika tiba na kuzuia magonjwa ya mzio (allergy) pamoja na pumu ya mapafu.
  • Hutibu tatizo la kupata choo kikavu au kutokupata choo (constipation)
  • Ni dawa nzuri sana kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
  • Husaidia katika matibabu na kuzuia mawe katika figo.
  • Hupunguza hatari ya kupata saratani ya mapafu, saratani ya utumbo na ugonjwa wa kisukari.
  • Huimarisha afya ya ini.
  • Husaidia figo kuondosha sumu aina ya uric acid ndani ya damu.

Matumizi na kipimo

  • Kwa ajili ya tiba kula matufaa kiasi cha kilo mbili kila siku kwa muda wa siku saba mfululizo.
  • Kunywa juisi ya matufaa bilauli moja kila baada ya saa nane kila siku.

Rejea

  • Benny P.J at al: A Review on the medicinal significance of common fruits. International J. of Biomedical Research Analysis, Sep-Oct 2010, vol.1, issue 2, pp.60-64.
  • Zhao P et al: Antitumor activities of apple extracts. Chinise Journal of Clinical Oncology 2006, 3(1):37-40.