Log in
Loving Hand for Disadvantaged and Aged (TZ)

Loving Hand for Disadvantaged and Aged (TZ)

Arusha, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Shirika hili lilianza rasimi mwaka 1998 na kusajiliwa mwaka 2000. Lilianza na watoto 12tu, kwenye kituo wakiwa na umri kati ya miaka 2 na 4. Hivi sasa lina watoto zaidi ya 150, vituo 3 na kimoja kiko Shinyanga, mahali ambako linajishughulisha na wazee waliokataliwa na jamii zao kwa tuhuma za kichawi.

Mafanikio makubwa tuliyoyapata kwa kipindi hicho ni kuwa na shule ya awali na msingi. Hivyo kurahisisha malezi kwa kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa mwenendo wa watoto.

Tumefanikiwa kuanzisha miradi midigo midogo ya pamoja kwa familia za watoto tunaowatunza hivyo kuwezesha familia hizi kutoa matunzo bora kwa watoto wao wakirudi nyumbani.