Envaya

kuhamasisha jamii

khamis chilinga (lindi)
2 Juni, 2011 12:10 EAT

asasi za kiraia ni tegemeo la jamii katika kuhamasisha na kusimamia miradi ya maendeleo katika kupeleka mbele ufanisi wa miradi kwenye maeneo yetu je tathmini na chukua hatua nini umefanya katika kipindi cha miezi sita mwaka huu kuelekea bajeti mpya ambayo inakuja katika halmashauri zetu?

JUMA MTI (DAR ES SALAAM)
8 Juni, 2011 12:05 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

Nimeweza kutoa mapendekezo ya halimashauri kuwa na mifuko maalumu kwa watoto yatima,watoto waishio katika mazingira hatarishi na wajane ili ziweze kuwasaidia katika elimu afya na kuanzisha miradi endelevu

BALTAZAR B KOMBA,(M2MWA WA WA2) (FAWOPA MTWARA)
9 Juni, 2011 20:26 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

NDUGU ZANGU WANAHARAKATI NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA UWEZEKANO WA KUINGIZA WAWAKILISHI WETU KATIKA MABARAZA YA MADIWANI NAMAANISHA KUWA NI VEMA NA NI HAKI YETU KUWA NA DIWANI KUTOKA KUNDI LA AZAKI KATIKA KILA HALMASHAULI,MBONA MBUNGE WA NGO YUPO INGAWA UWAKILISHI WAKE NI BANDIA NAYE TUANZE KUMJADILI MAPEMA,ILIFIKAPO UCHAGUZI UJAO TUSIWE WEKWEW TENA CHANGA LA MACHO NA ANNA ABDALAH ,NATUKIZUNGUMZA JUU YA BAJETI WAKATI HATUNA WAWAKILISHI KATIKA VIKAO VYA KUTOA MAAMUZI INAKUWA NI BURE KABISA.

Nicas Nibengo (BED-Mwanza)
10 Juni, 2011 00:16 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

Kwa kweli AZAKi zinahitaji kuwa na uwakilishi katika udiwani na ubunge.Hii itasaidia kusukuma mbele mjadala wa maendeleo na kushiriki katika maamuzi mbalimbali ya maendeleo

fikiri mvugaro (mwela theatre group temeke)
11 Juni, 2011 10:33 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

 kila kundi likidai uwakilishi patakua apatoshi lengo ni kuwepo na sheria za wazi zenye kutambulika na kama kiongozi akienda kinyme na sheria aweze kuadhibiwa kwa mfano kiongozi akiadi kuwa atajenga shule asame kwa mda gani na kwa bajeti hipi na kama akishidwa basi tumuadhibu kwa sheria hipi.kila siku tunalilia uwakilishi hao wanaotuakilisha wanatoka huku wananjaa wakila tu matulia bado tutakuwa atujapata ufumbuzi sheria hikiwa juu na uongozi na mavazi ya watu yakiwa chini kila mmoja atakuwa na haki maana imefika wakati mtu mwenye vazi furani au cheo furani hata akifanya kosa anagopwa asanteni sana

NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA)
12 Juni, 2011 12:33 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

 Pension jamii ni utaratibu endelevu wa kuwapatia wazee wote fedha tasilimu bila kuchangia,hii inaweza kufanyika kila baada ya muda uliokubaliwa,mfano kila mwezi au robo mwaka, mara nyingi fedha hizi hutolewa na serikali, kwa tafasili pana ni hatua au tendo la serikali au jamii kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa watu kuwawezesha kukabiliana na Majanga,hali ya kutojiweza na umasikini.HelpAge International ikishirikiana na NABROHO SOCIETY FOR THE AGED ya Mkoa wa Mwanza tunakampaini kubwa ya kuishawishi serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ianze kuwapatia wazee wote Pension Jamii ifikapo mwishoni mwa Mwaka huu bila kujari mzee huyo alifanya kazi serikalini au unadhani jambo hili linawezekana na nimhimu kwa wakati huu kama njia ya kuwapunguzia umasikini wazee?

 

Community Empowerment Foundation (COEF) (Kigamboni, Dar es Salaam)
15 Juni, 2011 13:18 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

Wananchi tunasikia mjadala juu ya hoja ya kukatwa posho za vikao vya wabunge na pesa kuhamishiwa katika masuala mengine ya maendeleo. Kundi la watawala wanatetea posho hizi zisiguswe.  Maudhui makubwa ni kwamba  KUNDI LA WATU WACHACHE WENYE DHAMANA YA KUONGOZA wanafikiria zaidi namna ya kujinufaisha na kujilimbikizia mali huku wakiacha kundi kubwa wanaloliongoza likiendelea kuzama katika lindi la umaskini.  Hawa ndio wabunge tulionao na Spika wetu.

 Wanaharakati tujadili na tuelimishane juu ya athari za mfumo unaosababisha mgawanyo wa raslimali za taifa usio wa haki pamoja na mikakati ya kuondokana na mfumo huu. Wabunge kulipwa zaidi ya mara moja kwa kazi moja ni ufisadi. Una mawazo gani juu ya hoja hii?

khamis chilinga (lindi)
15 Juni, 2011 18:09 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

posho,posho.posho ni alama kwamba sasa tuko katika karne ya posho na ukiigusa hiyo ujue utagombana na wengi.najua hata zito hana nia ya kuacha posho lakini nia yake kuonesha namna gani viongozi wetu roho zao zipo hapo ndio maana akaigusa na kweli amefanikiwa kwani mafisadi wote wameng"aka kwa kuogopa kupokonywa kula.posho kubwa kuliko kima cha chini cha mshahara ndio mbio zote za mwezi october mlikuwa mnakimbilia hapo!!!


Ongeza Ujumbe Mpya

Karibisha watu kushiriki