Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

FCS Narrative Report

Introduction

Lindi Region Association of Non Governmental Organizations
LANGO
Kufuatilia Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) za Mfuko wa Barabara za Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi
FCS/MG/1/11/167
Dates: 01 Septemba, 2011Quarter(s): 30 Novemba, 2011
Sharifu Maloya
S.L.P. 554
LINDI
Simu Mezani: +255 23 220 2108
Simu Kiganjani: +255 787 187 008;
+255 712 316 141
+255 762 565 383
Barua Pepe: smaloya22@yahoo.com
smaloya@hotmail.co.uk

Project Description

Governance and Accountability
Mradi wa Kujenga uwezo wa Jamii katika Kufuatilia Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) za sekta ya barabara za Serikali za Mitaa katika Halmasahauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi unalenga na kukusudia kuongeza uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika matumizi ya fedha na raslimali zinazotengwa na Serikali Kuu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Mfuko wa Fedha za Barabara (Road Fund) kwa lengo la kuimarisha na kuboresha miundombinu ya barabara mijini na vijijini.

Mradi unakidhi eneo la ufadhili la Utawala Bora na Uwajibikaji kwa kuwa mradi utajihusisha zaidi katika kupata taarifa kuhusu ni kiasi gani cha fedha zimepokelewa na Mamlaka hizo kwa miaka miwili hadi mitatu iliyopita kuotoka Serikali Kuu. Kisha wadau waliojengewa maarifa na stadi za kufanya ufuatiliaji, ukusanyaji taarifa, uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa na uandishi wa taarifa watatembelea miradi ya barabara iliyojengwa na/au kukarabatiwa kwa kutumia fedha hizo kati ya 3 hadi 5 kwa kila Halmashauri ya wilaya/Manispaa. Hatimaye taarifa zilizokusanywa kutoka kwa wananchi (jamii) walionufaika na miradi hiyo, watendaji wa serikali za mitaa, viongozi (Madiwani), Wakandarasi na wadau wengine wa maendeleo zitafanyiwa uchambuzi yakinifu. Rasimu za taarifa kutokana na uchambuzi zitaandaliwa kwa ajili ya kuhakikiwa na kuhaririwa ili hatimaye kufanyike mikutano ya mirejesho kwa wadau tofauti wa maendeleo waliopo katika Halmashauri husika ili kujionea mafanikio, mapungufu, changamoto na hatimaye kuibuliwa kwa mikakati ya pamoja ya kuhakikisha fedha na raslimali za umma zinatumika ipasavyo na kwa maslahi ya umma. Pia kuchochea upatikanaji wa habari na taarifa kuhusu miradi na shughuli za maendeleo kwa wananchi kutoka kwa viongozi na watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutumia mbao za matangazo, waandishi wa habari na vyombo vya habari kiujumla.

Kwa kufanya hivyo tunaamini kwamba ushiriki wa wananchi katika kufuatilia na kusimamia matumizi sahihi na bora ya fedha na raslimali za umma utaongezeka, kuimarika na kuboreka. Pia utendaji na uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa serikali za mitaa vitaimarika, kuboreka na kuleta tija na mafanikio makubwa kwa wananchi kwa maendeleo endelevu ya vizazi vya sasa na vijavyo.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLindi Manispaa - - 4200
LindiLindi Vijijini - - 4200
LindiLiwale - - 4200
LindiNachingwea - - 4200
LindiKilwa - - 4200
LindiRuangwa - - 4200
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female63812760
Male56211240
Total120024000

Project Outputs and Activities

1. Viongozi na Watendaji 42 wa Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi wameongezewa uelewa kuhusu ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma za sekta ya barabara.

2. Kuongezeka na kuimarika kwa uwezo wa AZAKi, Vyombo vya Habari na Jamii katika kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) katika sekta ya barabara za Serikali za Mitaa.

3. Kamati 6 zenye washiriki 30 za Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi zimefanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma katika sekta ya barabara.

4. Wadau 150 toka Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi wameshiriki Mikutano 6 ya mirejesho ya taarifa za ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya barabara za Serikali za Mitaa.

5. Machapisho ya Mabango 500, Kalenda 582 na Fulana (T-Shirts) 200 vyenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta ya barabara za serikali za mitaa vimechapishwa na kusambazwa katika Halamshauri 6 za Wilaya/Manispaa Mkoani Lindi.

6. Vipindi 12 na Matangazo mafupi 34 ya redio yameandaliwa na kurushwa kwa wananchi wa Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi na kwingineko kuhusu umuhimu wa jamii kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya barabara za Serikali za Mitaa.

7. Walengwa na wadau 180 toka Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi wameshiriki ufutiliaji na tathmni za maendeleo ya utekelezaji wa mradi na kubainika kwa mafanikio, mapungufu, changamoto na kuwepo kwa mikakati ya kuboresha utekelezaji wa mradi.

8. Walengwa na wadau 30 toka Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi wameshiriki tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi na kubainika kwa mafanikio (matokeo na mabadiliko), mapungufu, changamoto zilizojitokeza na mikakati ya kuhakikisha mradi unakuwa endelevu imeibuliwa.
1. Kufanya vikao 6 na viongozi (Madiwani) na Watendaji 42 wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi kuelezea malengo ya mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya barabara za Serikali za Mitaa Mkoani Lindi ifikapo Juni, 2012.

2. Mafunzo ya siku 3 kwa AZAKi, Waandishi wa Habari, Viongozi wa dini, Madiwani, na Watendaji wa LGAs wapatao 30 kutoka Halmshauri 6 za Wilaya/Manispaa Mkoani Lindi juu ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) za Miundombinu ya barabara ifikapo Juni, 2012.

3. Kuchapisha na kusambaza Mabango 500, Kalenda 582 na Fulana (T-Shirts) 200 vyenye ujumbe wa dhana na dhima ya PETS katika Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi ifikapo Juni, 2012.

4. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi katika Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi ifikapo Juni, 2012.

5. Kufanya gharama za Utawala na Uendeshaji wa Mradi.
1. Mradi umetambulishwa na kuelezewa malengo yake kwa madiwani na watendaji 42 wa Halmashauri 6 za Wilaya na Manispaa za Mkoa wa Lindi.

2. Wawakilishi wa AZAKi, Madiwani, Watendaji wa Kata na Waandishi wa Habari 30 toka Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi wamehudhuria mafunzo na kujengewa uwezo kimaarifa na kistadi katika kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika Halmashauri husika.

3. Mabango 500, Kalenda 582 na Fulana 200 vimechapishwa na kusambazwa katika Halmashauri 6 za wilaya/amanispaa za Mkoa wa Lindi vyenye ujumbe kuhusu umuhimu wa wananchi kushiriki kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya barabara na nyinginezo.

4. Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi zimefanyiwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi.

5. Mahitaji, vifaa na vitendea kazi vya ofisi ya LANGO na utekelezaji wa mradi kama vile; Kamera ya Dijitali, Kompyuta, Printa, Nukushi, Pikipiki na shajala vimenunuliwa na vinatumika kurahisisha na kuboresha utendaji wa kazi za kila siku na kuwezesha kufanikisha utekelezaji wa mradi.
Hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza katika utekelezaji wa shughuli za mradi.
1. Kufanya vikao vya kutambulisha na kuelezea malengo ya mradi - TZS. 2,226,000/=

2. Mafunzo juu ya dhana na dhima ya PETS kwa wadau - TZS. 4,913,000/=

3. Kuchapisha/kusambaza Mabango, Kalenda na Fulana (T-shirts) - TZS. 5,446,000/=

4. Kufanya ufuatiliaji / tathmini ya maendeleo ya utekelezaji mradi - TZS. 1,092, 000/=

5. Gharama za utawala na uendeshaji wa mradi - TZS. 7,170,000/=

Project Outcomes and Impact

1. Kuimarika na kuboreka kwa miundombinu ya barabara za mijini na vijijini katika Halmashauri zote 6 za Wilaya/Manispaa za Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Lindi ifikapo Juni 2012.

2. Kuongezeka kwa uwezo na ushiriki wa wadau wa maendeleo katika kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta ya barabara za Serikali za Mitaa katika wilaya/Manispaa 6 za Mkoa wa Lindi na kuboreka kwa uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa fedha na raslimali za sekta ya barabara ifikapo Juni, 2012.
1. Kuongezeka kwa uelewa na ufahamu wa baadhi ya Madiwani, Wakurugenzi watendaji, watendaji wa kata toka Halmashauri 6 za wilaya/manispaa kuhusu dhana na dhima ya ufuatiliaji (PETS) na umuhimu wake kwa utekelezaji fanisi na kuongezeka kwa tija katika kuchochea maendeleo ya wananchi.

2. Kuimarika na kuboreka kwa ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi na watendaji wa serikali za mitaa na asasi za kiraia katika michakato ya maendeleo.

3. Kuimarika kwa ushirikiano baina ya asasi za kiraia na waandishi wa habari katika kuhabarisha jamii kuhusu mradi na kushiriki katika kamati za PETS za kila wilaya.

4. Kuimarika na kuboreka kwa ushirikiano na mahusiano ya kiubia katika michakato ya maendeleo baina ya Serikali na Asasi za Kiraia.

5. Kuwepo kwa unganiko la kikazi kati ya Viongozi na Watendaji wa Serikali, wawakilisghi wa AZAKi na Waandishi wa Vyombo vya Habari tofauti katika kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta ya barabara katika kila wilaya/halmashauri husika.
1. Wadau wa maendeleo waliounda kamati za PETS za kila wilaya/Halmashauri kuwa na shauku na hamasa kubwa ya kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya barabara zilizopo chini ya serikali za mitaa licha ya muda wa kufanya hivyo kuwa bado haujafikia.
Hakuna sababu zozote zilizojitokeza zilizoleta na kupelekea tofauti ya mabadiliko.

Lessons Learned

Explanation
Viongozi na Watendaji wa Serikali za Mitaa wanahitaji kujengewa uwezo na ufahamu zaidi kuhusu umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika kufuatilia na kusimamia matumizi ya fedha na raslimali za umma katika miradi na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika maeneo yao.
Serikali ikipatiwa ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau wa maendeleo zikiwemo Asasi za Kiraia katika kufuatilia na kusimamia utekelezaji fanisi na wenye wa miradi na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika ngazi tofauti za Mamlaka za Serikali za Mitaa itaweza kuongeza kiwango cha uwazi, uwajibikaji, utawala wa sheria na bora katika michakato ya maendeleo..
Ni vyema na muhimu sana Asasi za Kiraia kushirikiana na Vyombo vya habari katika kujenga uwezo na kuongeza ufahamu wa jamii katika kutambua haki na wajibu wa kushiriki, kufuatilia na kusimamia miradi na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika maeneo yao ili kupunguza au kudhibiti kabisa matumizi mabaya ya fedha na raslimali za umma katika miradi/shughuli za maendeleo..
Wadau wa maendeleo na wananchi kiujumla wana shauku na hamu kubwa ya kujionea na kujiridhisha ni kwa kiwango gani cha ubora, ufanisi na tija kilichofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi au ukarabati wa barabara iliyotekelezwa na Serikali za Mitaa kupitia Mfuko wa Fedha za barabara (Road Fund) pamoja na sekta nyinginezo za maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Madiwani wanahitaji kusaidiwa kujengewa uwezo katika nyanja tofauti kuhusu Sera, Sheria, Mipango na Mikakati ya maendeleo tofauti ya kitaifa na kimataifa ili kuwawezesha kutambua na kusimamia utekelezaji wake katika ngazi tofauti za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha.
Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi zikitumia Radio za Kijamii zilizopo na zinazosikika katika maeneo yao ya kiutawala na kiutendaji ili kuhabarisha jamii kuhusu taarifa za kisera, kisheria, mikakati, mipango na bajeti za maendeleo pamoja na kiwango cha utekelezaji kilichofikiwa katika sekta na idara tofauti itasaidia na kuhamasisha wananchi kuziamini Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuzipatia ushirikiano wa dhati katika michakato mbalimbali ya maendeleo.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Dhana na dhima ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) bado haijafahamika vyema na viongozi, watendaji wa Serikali za Mitaa na wananchi kiujumla.Kuendelea kujenga uwezo na ufahamu zaidi kwa viongozi, watendaji wa serikali za mitaa na wananchi kiujumla kuhusu dhana na dhima ya ufuatiliaji matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS)
Washiriki wa mafunzo ya kujenga maarifa na stadi za ufuatiliaji matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) toka wilaya ya Liwale kudai malipo ya siku moja ya ziada kutokana na umbali toka Liwale hadi Lindi na hivyo kulazimika kulala Nachingwea wakati wa kurudi kutokana na hali ya miundombinu ya barabara na usafiri ilivyo.Washiriki toka wilaya ya Liwale walielimishwa na kuhamasishwa kuelewa kwamba bajeti ya mradi haiwezi kupanguliwa ghafla pasipo ruhusa ya mfadhili (FCS) kupitia kwa Afisa Ruzuku msimamizi.
Washiriki wa mafunzo ya PETS ambao ni Madiwani, wawakilishi wa AZAKi, Watendaji wa Kata na Waandishi wa Habari kuhitaji kwenda kufanya zoezi la ufuatiliaji baada ya kumalizika mafunzo kutokana na shauku na hamasa kubwa waliyonayo kujionea ubora na ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi au ukarabati wa barabara za mijini na vijijini licha ya muda muafaka wa kufanya hivyo kuwa bado kulingana na Mpango kazi wa utekelezaji mradi.. Washiriki wa mafunzo (Kamati za PETS) toka kila wilaya waliombwa kufanya subira kwa kuwa shughuli ya zoezi la ufuatiliaji inahusika katika robo ya pili ya mradi ambayo utekelezaji wake utafanyika baada ya kuandikwa na kuwasilishwa kwa ripoti za utekelezaji na fedha za mradi kwa mfadhili (FCS) na hatimaye kutolewa idhini ya kuendelea na utekelezaji shughuli za robo inafuatia licha ya fedha zake kuwepo akaunti benki.
Baadhi ya maeneo ya wilaya za Mkoa wa Lindi zina miundombinu ya barabara ambayo haiko katika hali nzuri na ya kuridhisha na hivyo kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuwa na ugumu/usumbufu kwa namna moja ama nyingine.Kutumia usafiri unaowezekana ikiwamo kukodi gari kutoka Wilaya ya Nachingwea kwenda Ruangwa ili kwenda sambamba na muda wakati wa utekelezaji wa shughuli ya utambulisho na kuelezea malengo ya mradi kwa viongozi na watendaji wa LGAs za Mkoa wa Lindi.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi.Kuhudhuria mafunzo ya kujenga maarifa na stadi katika kufanya ufuatiliaji (PETS) na kuunda kamati za PETS kwa wilaya/halmashauri husika.
Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi.Kupokea maelezo ya utambulisho na ufafanuzi wa malengo ya mradi na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika hatua zote muhimu za utekelezaji wa mradi ili kupata matokeo yaliyotarajiwa na kufikiwa kwa malengo yaliyokudiwa kikamilifu.
Baadhi ya Watendaji wa Kata wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi.Kuhudhuria mafunzo ya kujenga maarifa na stadi katika kufanya ufuatiliaji (PETS) na kuunda kamati za PETS kwa wilaya/halmashauri husika.
Waandishi wa Habari wa Magazeti, Radio na Televisheni kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi (LPC)Kuhudhuria mafunzo ya kujenga maarifa na stadi katika kufanya ufuatiliaji (PETS) na kuunda kamati za PETS kwa kila wilaya/halmashauri husika. Vilevile kuelimisha na kuhabarisha jamii taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi na umuhimu wake kwa maslahi pana ya umma.
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Lindi.Kuhudhuria mafunzo ya kujenga maarifa na stadi katika kufanya ufuatiliaji (PETS) na kuunda kamati za PETS kwa wilaya/halmashauri husika.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kufanya zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta ya barabara za serikali za mitaa katika miradi 18/30 ya halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi ifikapo Juni, 2012.xxxxxxxxxxxxxx
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi katika halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi ifikapo Juni, 2012.xxxxxxxxxxxxx
Kugharamia masuala ya kiutawala na uendeshaji wa shughuli za mradi.xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale20400
Male11220
Total31620
People living with HIV/AIDSFemale18360
Male13260
Total31620
ElderlyFemale1052100
Male981960
Total2034060
OrphansFemale631260
Male811620
Total1442880
ChildrenFemale1072140
Male871720
Total1943880
DisabledFemale12240
Male08160
Total20400
YouthFemale1142280
Male1022040
Total2164320
OtherFemale2044080
Male1573140
Total3617220
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku (MYG)Juni - Julai, 2011Jinsi ya kutekeleza mradi kiufanisi na kusimamia fedha za ruzuku kwa kuzingatia taratibu na sheria za fedha.Kutekeleza mradi sawa na mpango wa utekelezaji shughuli kwa kuzingatia taratibu na sheria za matumizi ya fedha.
Tamasha la Asasi za Kiraia 2011Novemba, 2011Umuhimu wa kubadilishana habari na taarifa tofauti za kisera, kisheria na maendeleo na utaandaaji.Kuziunganisha Asasi za Kiraia zenyewe pamoja na wadau wengine wa maendeleo kama vile; Serikali, Waandishi wa Habari n.k.
Mafunzo ya Uandaaji Mpango MkakatiJuni, 2011Jinsi ya kutayarisha Mpango Mkakati wa Asasi za KiraiaKuandaa rasimu ya Mpango Mkakati wa LANGO pamoja na Mipango mikakati ya Miandao ya AZAKi ya wilaya kwa kushirikiana na wanafunzi waliokuja kufanya mazoezi kwa vitendo kutoka Chuo Kikuu Dar (UDSM).
Mafunzo ya Uandishi wa Matokeo Bora ya Shughuli za AZAKi na utunzaji wa taarifa za shghuli/miradi.Aprili, 2011Jinsi ya kukusanya taarifa, kuzichambua na kuandika Matokeo Bora ya shughuli na miradi inayotekelezwa na AZAKiKuzishirikisha AZAKi kutambua na kuzingatia umuhimu wa kukusanya taarifa, kuzichamnua na kubainisha Matokeo Bora yaliyopatikana. Pia kuandaa rasimu ya Mradi ili kuombea ufadhili wa kujengea uwezo AZAKi katika uandishi wa Matokeo Bora

Attachments

« Previous

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.