Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Kufanya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi wa Vijiji 6 vilivyomo katika Kata ya Lundi Tarafa ya Matombo kuhusu mbinu za Ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za Ruzuku za Umma {PETS} zinazotengwa na serikali kwa ajili ya maboresho ya sekta ya Elimu.Pia tulifanya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Lundi na Wajumbe wa Kamati za Shule zilizomo katika kata ya Lundi juu ya Taratibu za Uandaaji wa Bajeti,Kanuni za Usimamizi wa fedha za Umma na Misingi ya Utawala Bora