Envaya
Parts of this page are in Swahili. View in English · Edit translations

Kwa sasa Asasi inashughulika na utafiti wa wanafunzi wa Kike ambao wameacha shule kutoka na kukosekana kwa ada na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha. katika Wilaya.utafiti huo utafanyika katika Wilaya ya Bagamoyo kama eneo la utafiti wa majaribio.

kazi hiyo kwa sasa inafanywa kwa kujitolea bado haijapatikana ufadhili au muhisani wa kufadhili shughuli hiyo.Utafiti huo unatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wasichana ambao walifaulu kujiunga na sekondari lakini wakaishia njia bila ya kutimiza malengo yao.

wakati programu hiyo ikiendelea asasi pia inawatembelea watu wanaoishi ya virusi vinavyosababisha UKIMWI katika kata ya Msata na Miono.Pia asasi inawasaidia wazee wasiojiweza 34 huduma za kibinadamu chakula na mahitaji mengine katika Kijiji cha Kihangaiko.

Asasi ya CHACODE kupitia idara ya habari na utafiti;hivi karibuni inatarajia kuendesha programu ya upashanaji wa habari kwa wananchi wanaoishi vijijini ili sauti zao ziweze kusikika,hasa ukizingatia ya kuwa mawasiliano ni kichocheo kikubwa cha maendeleo.Machapisho na sera mbalimbali za serikali zitaandikwa kwa lugha nyepesi bila ya kupoteza maana na lengo lililokusudiwa ili kuhakikisha ujumbe unawafikia walengwa katika viwango vyao mbalimbali vya elimu.

Pia asasi inatarajia kuanzisha jukwaa la vijana na changamoto za maendeleo ikiwa ni hatua ya kuelezea malengo yao na kitu gani wanafikiri kitakuwa kutatua na kupunguza kero zao za maisha na hivyo kupunguza makali ya maisha.